Please Limited time Offer!

Mapambazuko Ya Machweo Kcse Questions

Get Also Quick Study Guide For ‘ THE SAMARITAN’ by John Lara

MASWALI ya Mapambazuko Ya Machweo

1. ..iwapo penzi hili litatia doa, basi nirudishie mfuko huu kama ishara ya kulitupa penzi langu kama jongoo na mti wake…”

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili.                                                  (alama 4)
  2. Fafanua mbinu mbili ambazo zimetumika katika dondoo hili. 

(alama 4)

c) Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya.    (alama 6)

d) Eleza umuhimu wa msemewa wa hadithi hii katika kujenga ploti. 

(alama 6)

2. Kwa kurejelea hadithi zifuatazo, jadili maudhui ya nafasi ya vijana katika jamii.                                                                                  (alama 20)

i. Toba ya kalia  ii. Ahadi ni deni iii. 

iii. Nilitamani  iv. Pupa

3. Wanaume katika mataifa mengi barani afrika wametawaliwa na ubabedume. Jadili kauli hii ukirejelea hadithi ya “Fadhila za Punda” (al.20)

4. Huku ukitolea mifano mwafaka ,eleza jinsi ambavyo haki za watoto/vijana zimekiukwa katika hadithi ya Mapambazuko ya Machweo (alama 20)

5. Mwandishi katika hadithi ya Msiba wa Kujitakia alifaulu kutumia mbinu ya uwili. Thibitisha.                                                           (al. 20)

6. Mwandishi wa hadithi ya “mapambazuko ya machweo” uwajibikaji kwa kiasi kikubwa mno. Illihirisha ukweli na kauli hii   

                                                                                                                  (alama 20)

MASWALI ya Mapambazuko Ya Machweo

7. Wafanyikazi katika nchi nyingi zinazoendelea wanakumbwa na changamoto nyingi sana. Thibitisha hali hii kwa kurejelea hadithi ya ” harubu ya Maisha

                                                                                                                  (alama 20)

8. Ukombozi wa wanawake unakumbwa na vizingiti vingi sana. Jadili ukweli wa kauli hii ukirejelea hadithi ya sabina. 

                                                                                                                    (alama 20)

9. Fafanua changamoto wanazokumbana nazo waajiriwa katika hadithi Harubu ya Maisha                                                              (alama 20)

10. NDOA ni taasisi iliyokuzwa katika hadithi fadhila za punda. Fafanua  alama 20 

11. “mwanangu, nizike duniani unifunike…”   

i) Fafanua muktadha wa maneno haya.                                        (al.4)

ii)      Taja na utolee mfano mbinu moja ya kimtindo inayojitokeza katika dondoo hili                                   (al.2)

iii) Ukirejelea hadithi ya” Mzimu wa Kipwerere,” Fafanua jinsi imani katika mambo ya kichawi yamejikita katika jamii.                (al.14)

12. Fafanua jinsi mwanamke alivyosawiriwa katika hadithi ya Nipe nafasi 

alama 20

13. “Thank you. U mteja wa pekee, unajua kuthamini huduma nzuri unapopewa.” 

i) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (al.4) 

ii)         Taja na ueleze mbinu mbili za kimtindo katika dondoo hili.(al.4)

iii) Kwa kurejelea hadithi ya “Kila Mchezea Wembe,” Fafanua changamoto zinazowakumba watumiaji wa vileo kupita kiasi. (al. 12)

14.         “…iwapo penzi hili litatia doa, basi nirudishie mfuko huu kama ishara ya kulitupa penzi langu kama )ongoo na mti wake… 

a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 

b) Fafanua mbinu mbili ambazo zimetumika katika dondoo hili. (ala 4)  

c) Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya. (alama 6) 

d) EIeza umuhimu wa msemewa wa hadithi hii katika kujenga ploti. (al 6) 

15. Kwa kurejelea hadithi ya Ahadi ni Deni, fafanua namna Uwajibikaji umejitokeza.                                                         (alama 20) 

MASWALI ya Mapambazuko Ya Machweo

16. “Kwa kweli, nimeungulika sana miaka yote hii kwa unyama tuliomtendea Jack.. .” 

Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 

Jadili umuhimu wa msemaji wa dondoo hili. (alama 6) 

Jadili ukatili aliokuwa ametendewa mhusika Jack kulingana na dondoo hili. (alama 5) 

Kwa kurejelea mhusika Jack, jadili maudhui ya nafasi ya vijana.

(alama 5)  

17. Onyesha namna mwandishi wa hadithi ya Nipe Nafasi alivyodokeza maudhui ya taasubi  ya kiume.  

18. …wajua siku hizi huwezi kuamini yeyote apitaye na hasa akiomba msaada au umekua kututapeli?” 

Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4) 

Eleza umuhimu wa msemewa wa maneno haya katika kujenga maudhui

kwenye hadithi hii. (alama 10) 

  • Eleza sifa za msemaji wa maneneo haya. (alama 5)

19. Kwa kurejelea hadithi zifuatazo, jadili maudhui ya nafasi ya vijana katika jamii. (alama   20)  

Toba ya Kalia 

Ahadi ni Deni 

Nilitamani  PUPA 

20. Rachel Wangari katika hadithi ya mapambazuko ametumia mbinu ya JAZANDA kwa   upana. Jadili                                          alama 20   

21. Swala la Elimu limepewa kipaumbele katika hadithi ya sabina.

  Jadili                                                                                             alama 20 

22. Fafanua jinsi Yusuf Shoka Hamad katika hadithi MZIMU WA    KIPWERERE ameshughulikia swala la ushirikina na unafiki alama 20  

MASWALI ya Mapambazuko Ya Machweo

23. Umaskini ni donda sugu katika hadithi kifo cha suluhu, huku ukitoa hoja ishirini jadili                                                                           alama 20  

24. Eleza jinsi ubabedume umejitokeza katika hadithi ya nipe nafasi                                                                                                            alama 20 

25. Fafanua Changamato Wanazo Kumbana Nazo Waajiriwa Katika Hadithi

Harubu Ya   Maisha                                                                                  Alama 20

26. Jadili Matumizi Ya Pombe Haramu Na Athari Zake Katika Hadithi Kila

Mchezea  Wembe                                                                            Alama 20 

27. Fafanua wa ufaafu wa anwani Fadhila za Punda     (alama 20)

28. NDOA ni taasisi iliyokuzwa katika hadithi fadhila za punda. Fafanua 

alama 20 

MASWALI ya Mapambazuko Ya Machweo

29. Fafanua Dhiki/Changamoto Zinazowakumba Raia Katika Hadithi Msiba Wa Kujitakia  

30. Jadili ufaafu wa anwani Mapambazuko ya Machweo        (alama 20)

31. Fafanua dhana ya AJIRA katika hadithi mapambazuko ya machweo 

alama 20 

32. Urumo umekita mzizi katika jumuiya ya Mapambazuko ya Machweo.

             Jadili                                                                                           (alama 20)

33. Miti katika misitu ilizidi kuangamizwa kwa makali ya shoka lakini miti ilizidi kulifurahia shoka…miti ikafikiri shoka ni mmoja wao!”

 (alama 20)

  • a) Kwa kuzingatia hadithi ya harubu ya maisha, jadili changamoto

zinazokumba asasi ya ndoa.                                                                    (alama 5)

  • Kwa kuzingatia hadithi ya harubu ya maisha, fafanua matatizo

yanayowakumba wafanyikazi.                                                      (alama 10)

  • Jadili dhana ya utatu inavyojitokeza katika diwani ya mapambazuko ya

machweo na hadithi nyingine.                                                                 (alama 5)

35. tafadhali nisamehe…ni barua ilinikawiza…”

  1. Eleza muktadha wa dondoo hii.                                   (alama 4)
  2. Tambua kipengele kimoja cha kifani kilichotumiwa katika dondoo hili.

                                                                                                                  (alama 2)

  • Eleza barua hii na matokeo yake.                                          Alama 6)
  • Jadili dhima ya msemaji katika kuendeleza maudhui ya hadithi. 

(alama 8)

Possible KCSE Essay Questions and Answers To A Silent Song And Other Stories

Scroll to Top