Please Limited time Offer!

‘Bembea Yamaisha’by John W. Wanjala Possible KCSE Questions

Maswali ya Bembea Yamaisha

Get also Guide To An Artist Of The Floating World By Kazuo Ishiguro

  1. Mwandishi wa Bembea ya Maisha ameipa uzito mbinu rejeshi. Eleza. 

(alama 20) 

2. Soma dondoo hili na ujibu maswali. 

Mtu anaishi  na wanawe ambao wiki nzima anawaona wakiwa usingizini; wamelala fofofo.. .Nyumba ni ya yaya.” 

i. Weka maneno haya kwenye muktadha wake.                              (alama 4)  ii. Fafanua maudhui yanayojitokeza kwenye dondoo.                        (alama 2)  iii. Fafanua manufaa saba ya mazingira ya dondoo hili.                       (alama 14)  

3. Soma dondoo hili kisha ujibu maswali. 

Maisha yetu ni mfano wa mbegu iliyopandwa. Mbegu hiyo haina budi kuoza kwanza ndipo ioteshe mche upendezao. Mche huo wa asili ya mbegu iliyooza, hatimaye hutoa zao la mbegu nyingi ajabu. Ukitazama vizuri, mbegu ile haifi bali huchukua mkondo mwingine wa maisha. Huchukua umbo)ipya lipendezalo hasa ikiwa itakuwa imeangukia ardhi nzuri.. -Sasa rudini msaidie kuzalisha mbegu nyingi nzuri. Nyinyi mmebahatika kuwa mbegu nzuri istahiliyo kupandwa.” 

Hakiki ukweli wa maneno haya kwa kurejelea Bunju,Neema na wahudumu

                     hospitalini.                                                                                                        (alama 20) 

4. Bembea ya Maisha ni tamthilia inayohimiza mshikamano wa kijamii. Jadili. 

(alama 20) 

5. Mwanamke anaonyesha maumbo mbalimbali, mazuri na mabaya. Jadili 

(alama 20) 

6. Elimu ni mafundisho aali yatolewayo darasani au katika jamii. Jadili kwa

                     kurejelea tamthilia ya Bembea ya Maisha                                             (alama 20) 

‘Bembea Yamaisha’ Possible KCSE Questions

7. “Imani na itikadi huthaminiwa sana na jamii ya watu”. Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia ya bembea ya Maisha                     (alama 20)

8. Mwandishi wa tamthilia hii ameshughulia sana suala la Mabadiliko katika

                     jamii. Fafanua                                                                                                  (alama 20)

9. Eleza jinsi mwandishi watamthilia ya Bembea ya maisha alivyofanikiwa

                     kutumia ishara katika kazi yake                                                               (alama 20)

10. nwani bembea ya Maisha inaafiki tamthiliya hii. Jadili kwa kutoa hoja

                     ishirini                                                                                                                (alama 20)

11. Mila na desturi katika jamii zina umuhimu mkubwa kwa kuwa hutumika kama gundi inayoshikanisha jamii. Vilevile husaidia jamii kuwa na mwelekeo chanya na wa kimaendeleo. Hata hivyo, baadhi ya mila na desuri zinaweza kuzua migogoro katika jamii.                                               (alama 20)

12. A. Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali. 

‘Bembea Yamaisha’ Possible KCSE Questions

“La! Kila mbegu ipandwayo haina budi kuzaa na izaapo mazao yake huvunwa. Mtu huitakasa sahani akijua itamfaa tena. Kinacholelewa hakina budi kulea.” 

i. Fafanua muktadha wa mancno haya.                                                            (alama 4) 

ii. ii. Taja mbinu nne zilizotumika hapa.                                                   (alama 8) 

iii. iii. Eleza sifa nne za mnenaji                                                              (alama 8) 

13. A. Soma dondoo kisha ujibu maswali. 

“Kumbuka, mrina haogopi nyuki. Marehemu mamangu alizoea kutuambia kuwa nguvu hazimwishi mwanadamu wala hazipotei bure — humalizwa tu na mabuu. Mwanangu, usifanye hofu. Nikujuavyo mimi, hukuingia katika bahari si yako. Wala hakuna refu lisilokuwa na ncha. yote yana kikomo ati! Ipo siku haya yote yatapita. Mkulima hodari libasi yake huwa imechakaa na kuchoka lakini moyoni anabaki safl kama theluji kwa kutosheka na tija ya sulubu zake. Huwezi kumlinganisha na mkulima wa nguo safi zilizopigwa pasi zikanyooka.” 

i. Yaweke maneno haya katika muktadha wake.                              (alama 4)  ii. Fafanua sifa moja ya mnenaji inayojitokeza katika dondoo hili  (alama 2)  iii. Fafanua mbinu zilizotumika                                                                    (alama 8). 

           iv. Onyesha kuwa msemewa hakuingia bahari ambayo si yake          (alama 6)

14. Soma dondoo kisha ujibu maswali. 

Eti alama! My foot! Eti ameshuka nafasi darasani lakini akapandisha alama… 

  1. Eleza maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili.                                (alama 2)  
  2. Jadili sifa tano za mnenaji.                                                                   (alama 10) 

           iii,; Tathmini umuhimu wa mnenaji katika tamthilia.                              (alama 8)  

15. Soma dondoo kisha ujibu maswali. 

Ukilazwa tayari unakuwa umeonja seli,: Hata wahudumu wenyewe hawana mlahaka mwema. Amri na vitisho kama askari. Unashindwa kama UUguze moyo ama ugonjwa. Katika wodi hewa iliyojaa harufu ya dawa imezagaa, vitanda vimesalimu amri mpaka shiti zikagura. Yaani hali nzima haikupi matumaini ya kutoka ukiwa bora. Matumaini yanadidimia. Tumaini lako unaliweka katika sala. 

i: Changanua mtindo wa dondoo kwa kurejelea hoja tano.                      (alama 10)

‘Bembea Yamaisha’ Possible KCSE Questions

  ii. Fafanua namna mandhari ya dondoo hili yalivyochangia usukaji wa tamthilia. 

(alama 10) 

16. Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali.

‘...wanajikuta katika vuta n’kuvute inayochochewa na mitazamo ya kitamaduni, uhalisia wa mambo pamoja na matamanio ya wahusika binafsi. Baina yao kuna mitikiso inayotishia familia, ndoa na mahusiano ya kijamii. Kuna shutma, shaka, tuhuma na mivutano. Lakini pia kuna hongera, imani, ushirikiano, upendo, kutanabahi, na mshikamano. Katika huu mseto wa mambo ipo sauti imara.. .” 

i. Fafanua muktadha wa maneno haya.      (alama 4)

 ii. Hakiki mtindo wa dondoo hili.       (alama 2)

iii. Fafanua mitikiso saba inayotishia mahusiano ya 

Mwongozo Wa Bembea ya Maisha-Comprehensive Guide

Scroll to Top