Please Limited time Offer!

Kiswahili Form 3 Questions and Answers End Term 1 Exam Free

Kiswahili Form 3 Past Paper Questions with Marking Scheme

Kiswahili Kidato cha Tatu Maswali: Soma ufahamu ufuatao kasha ujibu maswali.

                                    Nafasi ya utafiti wa Kiswahili

Maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia yamezifikia jamii nyingi za Afrika na maeneo mengine yanayoendelea kupitia kwa lugha za kigeni, kama vile, Kiingereza na Kifaransa, na kupitia ushirikiano wa sehemu hizi na jamii za kimagharibi. Kutokana na hali hiyo, lugha zilizotumika na zinazoendelea kutumika katika mawasiliano ya kisayansi na kiteknolojia ni hizo za kimagharibi. Wakati uo huo, tunalo jukumu la kuwashirikisha wananchi wengi, ambao hawazijui lugha hizo, katika harakati hizi za kimaendeleo ya kisayansi ya pekee na kiteknolojia. Matumaini tuliyonayo ya kutuwezesha kufikia lengo hilo ni ya kuendeleza lugha zetu ambazo zaeleweka na wengi.

Kwa bahati nzuri, teknolojia mpya zinazoibuka pamoja na zile ambazo sasa zimekuwa zikitumika kwa muda hazikunuiwa lugha maalum. Lugha yoyote iwayo yaweza kutumika katika vyombo hivyo. Jambo hilo linasisitizwa na Mazrui na Mazrui (1995) ambao haiwezi ikayamudu mambo ya kisasa katika sayansi na teknolojia. Hata hivyo matumizi ya Kiswahili katika mitambo ya kisasa ya mawasiliano ni finyu mno. Panahitajika harakati madhubuti na mahsusi za kuiwezesha itumike zaidi katika vyombo hivi na hili litawezekana tu kupitia kwa juhudi za utafiti.

Manufaa ya mtambo wa kompyuta katika maisha ya sasa ni mengi mno. Hivi sasa kompyuta zinatumika katika sehemu mbalimbali za ulimwengu katika mpango wa elimu ya masafa. Mfumo wa mawasiliano ya mtandao, ambao kimsingi unajumuisha uunganishaji wa kompyuta nyingi duniani, umerahisisha sana ubadilishanaji wa habari. Utafiti wa Kiswahili unaweza kufaidika sana kupitia kwa mfumo huo kwa njia mbili kuu. Kwanza, kutokana na hifadhi kuu ya habari katika mfumo huo, mtafiti ataweza kupata habari mbalimbali kutoka kwa vianzo tofauti ambazo zitasaidia kufanikisha utafiti wake. Pili, itawezekana kufahamu ni maeneo gani ambayo yameshafanyiwa utafiti hapo awali na watafiti wengine. Kwa vile hatujaunganishwa vilivyo katika mfumo huo, mtafiti aweza akajitayarisha na kuupoteza muda mwingi kufanyia kipengele cha lugha ya Kiswahili utafiti na kumbe tayari kimeishatafitiwa kikamilifu. Aidha, tutaweza kupata fursa ya kujua matokeo ya tafiti mbalimbali  zilizofanywa kuhusu lugha ya Kiswahili. Hayo ni baadhi tu ya manufaa yanayopatikana kutokana na

maendeleo ya teknolojia ya habari ambayo kwa wasiojua lugha za kilimwengu kama Kiingereza hawayapati.

Katika karne hii ya Ishirini na Moja, vifaa vya mawasiliano vinaendelea kuwa changamano zaidi, huku mifumo ya uwasilishaji wa habari ya kisasa ya elektroniki ikiongezeka maradufu. Maendeleo haya ya mawasiliano yanapaswa kuendeleza utu na kuwaleta watu pamoja na wala si kuukengeusha umma. Hata hivyo, kuna tatizo la lugha.

Kwa kiasi kikubwa, maendeleo haya yanafanyika katika lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine za kilimwengu. Matokeo ni kuwa, kinyume na matarajio. Wengi wanaishia kukengeushwa; maana wanasikia tu uvumbuzi baada ya mwingine bila kujua hasa kilichovumbuliwa na manufaa yake kwao. Hali hii inadai utafiti wa kuziweka lugha zetu katika hali ya kufaidi maendeleo hayo. Maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia si milki ya wachache ambao wanaelewa Kiingereza, Kijerumani. au Kifaransa na kadhalika. Kwa upande wetu pa kuanzia si pengine bali ni kwa Kiswahili.

Ni wajibu wetu basi kuifanyia lugha hii utafiti wa kuiwezesha kutumika katika kufanikisha

mawasiliano kupitia kwa mitambo mipya ya kiteknolojia. Twapaswa kuangaza utafiti wetu katika nyanja mbalimbali za kisayansi na kiufundi ili ukosefu wa istalahi usiendelee kutolewa kama mojawapo ya sababu zizuiazo matumizi ya Kiswahili katika ngazi mbalimbali. Kuna umuhimu wa kuongeza kasi ya mradi wa utafiti utakaozalisha msamiati wa kompyuta; hali ambayo itapelekea kuwa na Kiswahili katika kompyuta; ambayo ni kiini cha vyombo vingine vingi vya mawasiliano ya kisasa

            Maswali

a)         Maendeleo ya kisayansi na teknolojia yamezifikiaje jamii nyingi za kitaifa?                                                                                                                                    (alama 2)

b)         Lugha kuu za kiafrika zinawezaje kuchangia maendeleo?                  (alama 2)

c)         Kwa nini matumizi ya Kiswahili katika sayansi na teknolojia ni funyu?                                                                                                                                                       (alama 3)

d)        Kuimarisha kwa hadhi ya lugha ya Kiswahili katika utafiti kuna manufaa

gani?                                                                                                               (alama 4)

e)         Taja kikwazo kikuu katika kuimarisha Kiswahili kama lugha ya sayansi na

            teknolojia.                                                                                                     (alama 1)

f)          Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu.           (alama 3)

            i)          Madhubuti

            ii)        finyu

            iii)       kengeusha

.

Kiswahili Form 3 Maswali MUHTASARI

            Soma taarifa ifuatayo kisha jibu swali litakalofuata.

NGUVU ZA UMEME

Uvumbuzi wa nguvu za umeme umemfanya binadamu kurahisisha juhudi za kujipatia mahitaji yake. Jambo hili limeifanya dunia kuwa mahali pema zaidi pa kuishi. Kumekuwa na maendeleo, wala si kama enzi za mababu zetu zilizokuwa za giza. Kutokana na utafiti mwingi pamoja na majaribio mengi, njia chungu nzima za kutengeneza nguvu za umeme zimegunduliwa. Njia hizo zimepanuliwa na kusambazwa kote na hata zimetia fora. Aina za nguvu zinazotumiwa ni zile zinazotokana na maji, mvuke, jua, mafuta, upepo na hata samadi.

Umeme kutokana na maji ni maarufu sana ulimwenguni. Hii ndiyo njia ya kimsingi ya  nguvu za umeme. Bwawa hujengwa kwenye mto kuhifadhi maji. Mifereji inayotoa maji haya bwawani huelekezwa kwenye magurudumu yanayoviringishwa na nguvu za maji hayo. Magurudumu haya nayo huzungusha nyuzi za shaba zilizowekwa sumaku na hivyo hutoa aina moja ya kawi. Isitoshe, kawi hii hubadilishwa ili kupata nguvu za umeme zinazohitajika. Umeme unaopatikana husafirishwa kwa kutumia waya za shaba hadi kwenye vituo au sehemu zinazohitaji nguvu hizi. Nchini Kenya, vituo vinavyotoa stima-maji ni kama Kiambere, Wanjie, Turkwell, Masinga, Kamburu, Gitaru, na Kindaruma na vinginevyo.

Kutokana na milipuko ya volkeno pamoja na zilizala, njia nyingine ya kutengeneza nguvu za umeme imevumbuliwa. Njia hii inawezekana kwenye mahali palipo na chemchemi, za maji moto kama huko Olkaria na mifereji ya chuma huwekwa ili mvuke uelekezwe kwenye magurudumu yanayoviringishwa kasi na kutoa umeme.

Majenereta au vifanyiza vinavyotoa nguvu za umeme huonekana kila mahali nchini, hasa kwenye shule na hospitali. Majenereta haya hutumia mafuta ya aina ya taa, petroli au diseli. Kifanyiza kikiwashwa, mafuta haya huchomeka ndani ya injini ili kutoa nguvu za kuendesha mitambo ya kutengeneza umeme.

Stima-jua ni nguvu nyingine ambazo zimeanza kufanyiwa kampeni siku za hivi karibuni. Watu wamehimizwa kutumia, stima-jua kwa sababu jua angani, hutoa mwanga unaoambatana na joto kali, hasa katika sehemu za tropiki. Miale ya jua huangaza juu ya kioo kinachotengeneza nguvu hizi. Miale hii uelekezwa kwenye vidubwashadubwasha vilivyo chini ya kioo vinavyoibadilisha kuwa nguu za umeme. Joto kutoka juani hutumika kuchemsha maji na kutolea nguvu za umeme nyumbani. Pia, kuna umeme unaotokana na nguvu za tonoradi au nyukilia, lakini nguvu hizi hutumiwa na nchi chache sana, hasa zile zilizoendelea kama Urusi, Marekani, Uingereza, Ufaransa, Uchina, India, Israeli na Misri.

Samadi ya wanyama kama ng’ombe nayo hutumiwa kutengeneza aina moja ya kawi. Ikiwa katika hali ya majimaji, samadi hutiwa katika pipa maalum na kuongezewa maji, Matokeo yake ni gesi na joto linalotoa nguvu za umeme, ambavyo hupitia kwa kifaa kinachotiwa ndani ya pipa la samadi hiyo. Upepo na makaa ya mawe, pia hutumika kutengeneza nguvu za umeme katika sehemu zingine za ulimwengu.

MASWALI

a)         Eleza jinsi nguvu za umeme zinavyozalishwa.  (Maneno 55–60)

                        Matayarisho                                                                                      (alama 8)

..

                        Jibu

            b)         Fupisha aya ya pili kwa maneno (55 – 60)

                        Matayarisho

.

                        Jibu

.

Kiswahili F3 Maswali SEHEMU YA C: MATUMIZI YA LUGHA.

            a)         Eleza tofauti kati ya sauti /dh/na/th/                                            (alama.2)

            b)         Tunga sentensi mbili ukitumia ni kama kitenzi na kama kielezi.   (alama.2)

..

c)         Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo.                                                       (alama.2)

            i)          Walipokelewa wageni.

            ii)        Walipokezwa wageni.

d)        Andika wingi wa sentensi ifuatayo.

            Wakati wa kiangazi kuna tatizo linalokumba zaraa.                             (alama.2)

e)         Andika sentensi hii kwa usemi wa taifa.

Fatuma alisema, “Sofia alinitea nguo yake jana na nitaivaa kesho nikienda Nairobi.”                                                                                                                                           (alama.2)

f) Tofautisha matumizi ya ngali katika sentensi.

                        i)          Zarika angali anasoma.

                        ii)        Mwanafunzi angalisoma angalipita.                                (alama.2)

.

g) Bainisha aina za shamirisho katika sentensi hii .

            Shangazi alitumiwa baruanamjombangu kwa posta                             (alama.3)       

h) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya vishale.

Mganga aliyefarikijanaatazikwa kesho.                                                                           (al 4.)

i)Badilisha sentensi hii iwe katika hali ya udogo

Jipaka lilirarua jinguo lake.                                                                                         (alama.2)

j) Yakinisha.

Usingekuwa  na nia safi asingekusamehe                                                               (alama.2)

k)Sahihisha sentensi hii

Mtu ambaye anakula mkate ametumana aletewe chai.                                     (alama.2)

L) Andika sentensi mpya kwa kufuata maagizo

Kama watoto hawawathamini wazazi wao hawawezi kufanikiwa maishani.

            Anza Ni vigumu                                                                                 (alama .2)

M)       Akifisha:

Nani aliyekikata chandarua changu kwa wembe sasa sitaweza kusafiri nilikotaka kwenda kule malaba ninamtaka aje aniombe msamaha.                                    (alama.3)

N)        i)Eleza matumizi mawili ya kiambishi ndi-

ii)        Ainisha viambishi awali na tamati katika neno lifuatalo.

                        Wameridhiana.                                                                                    (alama.4)

O)        Tumia amba katika sentesi ifuatayo:

            Wanafunzi wapitao mtihani husherehekea.                                                   (alama.1)

p)Tumia kivumishi cha nomino kutunga sentensi.                                                   (alama.1)

q) Taja aina ya kirai kilichopigwa mstari katika sentensi ifuatayo.

                                    Walimu wa Kiswahili watawasili leo.                                    (alama.1)

r)Andika kinyume cha sentensi hii.

                        Mvulana mmoja ameoa.                                                                     (alama.1)

s) Sentensi zifuatazo ni za aina gani?

            i)          Aliyetoroka ni yule.

            ii)        Sisi ndisi wezi ilhali wale ni watundu.                                            (alama. 2.)

SEHEMU YA D: ISIMU JAMII (Alama 10)

 (a)       Eleza maana ya lugha ya taifa.                                                                   (alama 2)

 (b)      Eleza sababu tatu zinazofanya watu kubadili na kuchanganya ndimi.   (alama 3)

 (c)       Eleza hatua tano ambazo zimesaidia kukuza lugha ya Kiswahili baada ya uhuru nchini Kenya.                                                                                                            (alama 5)

Scroll to Top