For Answers call 0754238886
Nguu Za Jadi Possible KCSE Questions And Answers
QUESTION 1
‘‘Japo nilipungukiwa na mengi niliyotamani, nilitaka nyinyi muote mbawa mpae juu na
kuitazama dunia kutoka kule juu kwa niaba yangu. Stahamala yangu haikuniletea
hasara…’’
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b) Bainisha toni inayojitokeza katika dondoo hili (alama 2)
c) Eleza umuhimu wa mandhari ya dondoo hili (alama 8)
d) Onyesha namna stahamala ya msemaji ilimletea manufaa (alama 6)
QUESTION 2: Bembea Ya Maisha Questions
‘‘….Mara ile ya kuzuka, ulikuwa kimbaumbau mwiko wa pilau. Upepo kidogo tu
ungekuyumbisha kama jani kavu wakati wa kipupwe.’’
a) Tambua mbinu nne za kimtindo katika dondoo hili (alama 4 )
b) Onyesha namna wahusika mbalimbali walivyoyumbishwa na hali tofauti katika
tamthilia (alama 10)
c) Eleza umuhimu wa msemaji wa maneno haya katika kukuza : (alama 6)
i) ploti
ii) wahusika wengine
QUESTION 3: Bembea Ya Maisha Revision Questions
‘’Dunia ikijua anakusaidia jikoni itasema unashusha hadhi yake na kwa mizani ya jamii utakuwa unajivulia nguo. ‘’
a. Eleza muktadha wa maneno haya. Alama 4
b. Tambua tamathali mbili za usemi katika dondoo. Alama 2
c. Fafanua sifa zozote nne za msemaji wa maneno haya. Alama 4
d. Tathmini umuhimu wa mandhari kwa kurejelea nyumbani kwa Sara. Alama 10
QUESTION 4: Maswali Ya Bembea ya Maisha
‘’ Kila mbegu ipandwayo haina budi kuzaa na izaapo mazao yake huvunwa. Mtu
huitakasa sahani akijua itamfaa tena.’’
a. Eleza muktadha wa maneno haya. Alama 4
b. Fafanua umuhimu wa msemaji katika kujenga ploti. Alama 4
c. Tambua mbinu moja ya kimtindo katika dondoo. Alama 2
d. Kwa kutoa mifano kumi eleza namna mbinu iliyotambuliwa katika sehemu (c)
imetumiwa kuendeleza tamthilia hii. Alama 10
QUESTION 5 Mwaswali ya Mwongozo wa Bembea ya Maisha
Maisha ya sasa hayana fundi. Yanamwendesha kila mtu kama tawi lililosukumwa hadi
likang’oka kutoka taagani na kupeperushwa na upepo….Ulimwengu wa sasa haubagui.
Wadogo kwa wakubwa…..
a) Eleza mkutadha wa nukuu (alama 4)
b) Changanua vipengele vitano vya kimtindo katika nukuu (alama 5)
c) Fafanua mbinu nne za kutambua hulka za mneneji (alama 4)
d) ‘Maisha ya sasa hayana fundi.’ Fafanua mbinu ishi wanazotumia wahusika tamthiliani
kukabiliana na hali zao. (alama 7)
QUESTION 6
(a) Changanua mtindo katika kifungu kifuatacho. (alama 4)
Naam, bembea! Hata bembea ikiwa ya kamba au chuma hatimaye hulika. Wanasema papo kwa
papo kamba hukata jiwe. Bembea inapolika na kukatika haiwi mwisho wa mchezo. Huungwa na
mchezo kuanza tena.
(b) Eleza toni katika dondoo hili. (alama 2)
(c)Jadili umuhimu wa mandhari katika tamthilia hii (alama 6)
(d) (i) Fafanua kinaya katika kauli iliyopigiwa mstari (alama 1)
(ii) Dhihirisha kinaya katika kauli iliyopigiwa mstari kwa kurejelea tamthilia (alama 7)
QUESTION 7
a) Changanua mtindo katika kifungu hiki. ( alama 5)
“Bunju ni mmoja wenu.Nyote ni wanangu.Hayo ni maneno ya mama.Wakati huo sikuona.Sasa
ninaona.Wanasema mwenye macho haambiwi tazama.Kweli iliyoje!Japo hutokea wakati
tukalalamika.Ninafikiri Bunju ni zawadi nzuri kwetu.Leo tungekuwa wapi bila Bunju?Maji yangezidi
unga,usingepikika,usingelika.Hebu fikiri!Umepata ajali mbaya.Inakuacha mahututi.Anapita mtu katika gari
lake kwa Imani anaguswa.Anakufanyia mpango wa flying doctors..
b) Msemaji wa maneno haya ni kielelezo cha uwajibikaji.Fafanua. (alama 8)
c) Tambua toni katika kifungu hiki.( alama 2)
QUESTION 8
“Huko ndiko kuvumilia hasa. Tazama faraja ilivyoalika sasa.”
a) Weka dondoo hili katika muktadha. (alama 4)
b) Eleza sifa na umuhimu wa msemaji huyu katika Tamthilia ya Bembea ya maisha.
(alama 6)
c) Kwa kutolea hoja kumi onyesha jinsi faraja ilivyoalika katika maisha ya msemewa maneno kwenye dondoo. (alama 10)
QUESTION 9
a). Jadili maudhui ya utamaduni katika jamii ya Bembea ya maisha. (Al.10).
b). Fafanua sifa za mhusika Sara. (Al.10)
QUESTION 10 Maswali ya Bembea ya Maisha
“Asiyejua safari ya Sara na Yona akielezwa huiona kama ffilamu”.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.( alama 4)
b) Bainisha matumizi mawili ya mbinu za lugha zilizotumika katika dondoo hili.( alama 2)
c) Eleza sifa za msemewa.( alama 4)
d) Eleza umuhimu wa msemaji.( alama 5)
e) Eleza sifa za Yona kama zinavyojitokeza kwenye tamthiliya ya Bembea ya maisha.( alama
Download Swahili SetBooks Guides (Mwongozo)
Nguu Za Jadi Possible KCSE Questions And Answers