Ushairi KCSE Questions And Answers-Questions 6-10
USHAIRI WA 11
Soma shairi hili kisha ujibu maswali.
Jicho, tavumiliaje, kwa hayo uyaonayo?
Kicho, utasubirije, maonevu yapitayo
Kwacho, lijalo na lije, nimechoka vumiliyo
Naandika!
Moyo, unao timbuko, maudhi tuyasikiayo
Nayo, visa na mauko, wanyonge wayakutayo
Kwayo, sina zuiliko, natoa niyahisiyo
Naandika!
Hawa, wanotulimiya, dhiki wavumiliayo
Hawa, mamiya mamiya, na mali wazalishayo
Hawa, ndo wanaoumiya, na maafa wakutayo
Naandika!
Hawa, sioni wengine, kwao liko angamiyo
Hawa, uwapa unene, watukufu wenye nayo
Hawa, bado ni wavune, kwa shida waikutayo
Naandika!
Bado, wawapo mabwana, wenye pupa na kamiyo
Bado, tafauti sana, kwa pato na mengineyo
Bado, tuling’owe shina, ulaji pia na choyo
Naandika!
Maswali
- Shairi hili laweza kuwekwa katika bahari zipi? (alama 4)
Thibitisha kila jibu lako.
- Eleza dhamira ya mshairi. (alama 2)
- Onyesha mifano miwili ya uhuru wa kishairi jinsi ulivyotumika katika shairi. (alama 2)
- Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (alama 4)
- Tambulisha kwa mifano mbinu zozote mbili za sanaa katika shairi. (alama2)
- Fafanua sifa za kiarudhi zilizotumika katika ubeti wa tano. (alama 3)
- Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi. (alama 3)
(i) Zuiliko
(ii) Wavune
(iii) Wenye pupa na Kamiyo.
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 11
1. a) Tarbia – Lina mishororo minne katika kila ubeti
Msuko – Kibwagizo kimefupishwa.
Ukara – Vina vya nje vinatiririka katika beti zote ilhali vya
ndani havitiririki.
Ukawafi – Una vipande vitatu (ukwapi, utao na mwandamizi)
katika mishiroro ya kwanza mitatu ya kila ubeti isipokuwa kibwagizo
Kikwamba – Katika beti za 3-5 neno moja ndilo linaanza kila mshororo.
Sakarani – Kuna bahari kadhaa katika shairi.
- Kuwahimiza watu (hasa wanyonge P) wainuke na kupinga Pmaovu na maonevu wanayofanyiwa na matajiri wenye uwezo.
- Inkisari km vumiliyo – kuvumilia nanaandika.
Mazida kurefusha k.m. angamiyo, vumiliyo n.k.
Tabdila k.m mamiya badala ya mamia
- Hawa wanaotulimia wanavumiliaP dhiki
Wao ni wengi P na ndio huzalisha mali.
Wao ndio wanaoumiaP na kupata mateso / taabu
Wanayokumbana nayo.Ninaandika / ninasema
- Takriri – hawa, bado, mamiya.
Balagha – uyaonaje?
Taharuki – Naandika!
Inkisari – Hawa, ndo
Kinaya – Watukufu wenye nayo
f) Kuna mishororo minne
Kuna vipande vitatu katika mishororo ya kwanza mitatu na kimoja katika kibwagizo
Vina vinatiririka / vinafanana
Mizani 2,- 6-8
2-6-8
2 – 6 – 8
4
g) i) Cha kunizuia / kizuizi / kizingiti / uoga / hofu/ pingamizi
ii) Wachovu /dhaifu /hafifu
iii) Walio na tamaa kubwa / walafi/ mabwanyenye
SHAIRI LA 12
Soma shairi hili kisha ujibu mawali yanayofuata.
SABUNI YA ROHO
Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
Ndiwe suluhu la zama, waja wakukimbilia,
Waja wanakutazama, madeni wakalipia,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
Utanunua majoho, majumba na nyumbani,
Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Matajiri wakujua, wema wako wameonja,
Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
Sura Zao ‘mefufua, Wanazuru kila nyanja,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mvunja mlima, onana na masikini
Watazame mayatima, kwao kumekua wa duni
Wabebe waliokwama, wainue walio chini,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mvunja mlima,wapi kapata uwezo?
Umezua uhasama, waja kupata mizozo,
Ndiwe chanzo cha zahama, umewaitia vikwazo,
Ndiwe sabuni ya roho, Ndiwe mvunja mlima.
Umevunja usuhuba, familia zazozana,
Walokuwa mahabuba, kila mara wagombana,
Roho zao umekaba, majumbani wachinjana,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
Niondoe jehanamu, ya ufukara wa sumu,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika
Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
- Mshairi anaongea na nani katika shairi hili? [alama 1]
- Taja majina mengine matatu aliyopewa huyu anayesemeshwa. [alama 3]
- Anayezungumziwa katika shairi hili amesababisha balaa gani? [alama 2]
- Mshairi anatoa mwito gani kwa mwenziwe? [alama 4]
- Fafanua maudhui ya ubeti wa sita. [alama 2]
- Mbinu kadha za uandishi zimetumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe wake. Taja mbinu zozote tatu na uzitolee mifano katika shairi. [alama 3]
- Fafanua maana ya:
Sura zao “mefufua, wanazuru kila nyanja. [alama 1]
- Andika ubeti wa saba katika lugha nathari. [ alama 4]
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 12
1. (a) pesa.
(b)Majina aliyopewa.
- Sabuni ya roho.
- Mvunja mlima.
- Mafuta ya roho.
- Fulusi .
- Tunu ya mtima.
- Suluhu la zama.
(c) Amesababisha balaa gani.
- Amesababisha uhasama/ uadui.
- Ugomvi kati ya wapenzi.
- Vifo.
(d) Mtoto kwa mwenziwe.
- Awaarike maskini na mayatima .
- Asimwangamize bali bali amwondoe kwenye ufukara.
- Amwitapo aitike.
- Aache uchoyo / amtatulie shida zake.
- Amchekeshe /amfurahishe.
(e) Maudhui ya ubeti wa sita .
-Pesa zimezua uhasama katika ndoa nyingi na kusababisha vifo.
(f) Mbinu za uandishi.
- Istiara –Pesa ni sabuni/mafuta. n.k
- Semi – mvunja mlima.
— sabuni ya roho.
(iii) Tashhisi –umevunja usuhuba.
-umezua uhasama.
(iv)Balagha- kwa nini wanikimbia?
–wapi kapata uwezo?
(v)Takriri—Ndiwe mvunja mlima.
Mbinu na mfano alama 1
(g) Maana ya-
Sura zao imefufua, wanazuru kila nyanja.
-Pesa zimewaletea furaha hata wanatalii sehemu zozote wanazotaka.
Alama 1
(h)Lugha nathari.
Mashairi anasema kuwa anamtafuta pesa sana ili amsaide. Anamsihi asimpige kwa kumtoroka na kumwacha hoi bila uwezo. Anamwomba amuondoe katika lindi hili la umaskini kwa vile yeye ndiye anayetuliza watu na kuwaondolea matatizo ya kila namna. Alama 4
USHAIRI WA 13
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
- Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,
Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,
Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
- Dunia ingetatana, na kizazi katikati,
Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti,
Vipi tungeliona, na kuzaa hatuwati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
- Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti,
Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati,
Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
- Walakini subuhana, kapanga sisi na miti,
Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti,
Maisha ya kupishana, yule ende yule keti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
- Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti,
Kwa uwezewe Rabana, kaipanga madhubuti,
Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
- Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati ,
Sote tungeambatana, pa kulima hatupati,
Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
- Peleleza utaona, hayataki utafiti,
Kama tungelikongana , ingelikuwa ni bahati,
Vipi tungelisukumana, katika hiyo hayati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
- Mbele sitakwenda tena, hapa mwisho nasukuti,
Yaeleni waungwana, shauri yake jabaruti,
Yote tuloelezana, katenda bila senti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
MASWALI
a) Shairi hili ni la bahari gani? (alama 2)
b) kwa kutoa mifano mwafaka onyesha jinsi mtunzi wa shairi hili alivyotumia
uhuru wa utunzi (alama 2)
c) Eleza muundo wa shairi hili (alama 4)
c) Andika ubeti wa tano katika lugha nathari. (alama 4)
d) Tambulisha mbinu zozote mbili za lugha zilizotumiwa na mshairi (alama 4)
e) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika shairi
i)katiti
ii) yakuti
iii) Hatuwati
iv) Nasukuti (alama 4)
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 13
Bahari la shairi
- Tarbia au unne
- Mtirirko – vina vya kati na vya nje vinafafana katika shairi nzima.
Km vya kati vya mwisho
na ti
na ti
na ti
ti na
- Mathnawi- lina vipande viwili
Ukwapi na utao.
- Idhini / uhuru / ruhusa
- Inkisari km ngekuwa, ngetutafuna
- Tabdila km sharuti – sharti.
- Kuboronga sarufi – mauti kawa hakuna
– katika wote wakati
(iv) Lahaja – Hatuwati – Hatuwachi
Yaoleni – yaoneni
- Umbo /sura / muundo / mpangilio
- Beti 8
- Mishororo 4 kila ubeti / tarbia / unne
- Mizani 16 kila mshororo
- Mtiririko wa vina.
- Vipande viwili
- Kibwagizo kunachorudiwarudiwa
- Ujumbe katika ubeti wa 5
- Dunia haiwezi kujaa watu kupita kiasi.
- Mwenyezi mungu anajua kupanga
- Baadhi ya watu wale na baadhi wazaliwe.
- Bila kifo duniani tungesongomana
- Mbinu za lugha
- Balagha km – vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
- Tashbihi – ikawa kama yakuti kama ukosi na shati
- Takriri – si ati ati
- Maana.
(i) Katiti – kidogo / chache
(ii) Yakuti – kito cha thamani
(iii) Hatuwati – hatuwachi
(iv) Nasukuti – sirudi nyumi,
USHAIRI WA 14
KIFO
1. ‘likuwa tisini moja 2. ‘lituachia vioja
‘lipojikunja pamoja Raha hatujaionja
Kutuaga mara moja Tumezidi na kungoja
Safari moja kwa moja Matumaini ya waja.
3. Kifo hatuna faraja 4. Maisha ‘mekosa haja
Baba livuka daraja Na mama amejikunja
‘likuwa wetu kiranja katwa auma viganja
Majonzi ‘lituachia Nyumba sasa inavuja
5. Vitamu nani taonja 6. Kifo kwetu sisi waja
Mali sasa imefuja Tumaini hutuvunja
Mifupa tutaivunja Ingawa ndio daraja
Mifugo katu uwanja Haituweki pamoja
MASWALI
1. Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
2. Mshairi ana ujumbe gani ? (alama 2)
3. Taja mbinu zozote tatu za lugha alizotumia mshairi na uzitolee mifano kutoka shairi.(alama 6)
4. Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (alama 4)
5. Eleza maana ya mistari hii kama ilivyotumika katika shairi. (alama 2)
i) Baba livuka daraja
- Kutwa auma viganja
6. i) Mshairi ametumia mbinu gani katika maneno haya . (alama 1)
‘likuwa
‘lituachia
‘lipojikunja
ii) Kwa nini akatumia mbinu hiyo? (alama 1)
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA SHAIRI LA 14
- – Beti -6
– Mishororo 4 kila ubeti
– mizani 8 kila mshororo
– Kipokeo kinatofautiana kila ubeti
– Utenzi
2. – Kifo ndio daraja ya kila mtu
– kifo huacha watu bila matumaini
– hufanya watu wateseke
3. – Takriri – moja
– Tashhisi – kifo
– Taswira
– Tunia – fuja, vunja
4. – Hawana raha baba alipofariki aliwekuwa kiongozi wao sasa amewaachia shida tupu.
5. – Alifariki
– Anajuta
6. – Inkisani – idadi ya mizani iwe sawa / urari wa mizani
USHAIRI WA 15
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yote.
KIPIMO NI KIPI?
Nitampa nani, sauti yangu ya dhati
Kwa kipimo gani, ingawa kiwe katiti
Amefanya nini, La kutetea umati
Kipimo ni kipi?
Yupi wa maani, asosita katikati
Alo na maoni, yasojua gatigati
Atazame chini, kwa kile ule wakati
Kipimo ni kipi?
Alo mzalendo, atambuaye shuruti
Asiye mafundo, asojua mangiriti
Anoshika pendo, hata katika mauti
Kipimo ni kipi?
Kipimo ni kipi, changu mimi kudhibiti
Utu uko wapi, ni wapi unapoketi
Nije kwa mkwapi, au ndani kwa buheti
Kipimo ni kipi?
- Eleza umbo la shairi hili Alama 4
- Taja tamadhaliza usemi na kisha utoe mifano Alama 3
- Taja na ueleze namna mshairi alivyotumia uhuru wa ushairi? Alama 2
- Eleza maudhui ya shairi hili? Alama 3
- Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari Alama 4
- Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa Alama 4
- Katiti
- Gatigati
- Shuruti
- Mangiriti
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 15
- Tarbia –lina mishororo minne.
- Vina vya ndani havitiririki –vina vya nje vinatiririka.
- Mizani 6-8
6-8
6-8
8
- Lina kibwagizo –kipimo ni kipi?
- Vipande viwili isipokuwa kibwagizo.
Alama 4
- Balagha –kipimo ni kipi?
- Usemi –atazame chini.
- Tashhisi –kukipa kitu kisicho na uhai. (maoni yasojua gatigati)
- Inkisari- asosita –asiyesita
-alo -aliye
-yasojua -yasiojua
-anoshika-anayeshika
Tabdila-maani-maana
- Watu wapende nchi yao kwa kufuata sheria zake.
- Watu wasichukue watu wengine.
- Watu hawana utu.
- Hana uhuru wa kutoa maoni.
Apendaye nchi yake na kufuata
Sheria zake, asiyechukia watu wala kuhadaa,
Kudanganya, au yule ashikaye
Pendo hadi kifoni, atajulikanaje au atapimwaje? Alama 4
- Katiti –kidogo.
Gatigati –ubaguzi/upendeleo.
Shuruti –lazima.
Mangiriti –mambo ya kuhadaa/uongo.