Please Limited time Offer!

Ushairi KCSE Questions And Answers-Questions 1-5

Ushairi KCSE Questions And Answers-Questions 6-10

Mwongozo Wa Ushairi- Questions and Answers

USHAIRI WA 1

Soma shairi lifuatalo kwa makini halafu ujibu maswali yanayofuata

  1. Naja sasa ni ndiyani, naja kwetu Mzalendo

Naja nirudi nyumbani, nilowekwa nako kando

Kwetu’ mi nakutamani, kulo na mwingi uhondo

Nijaye ni yule nyundo, misumari hadharini

  1. Naja kwingine kuwapi, kulojaa langu pendo?

Huenda nende kwinginepi, sawa nako kwa muundo?

Kaa kwingine anapi, ela kwenye lakwe gando?

Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini

  1. Naja nije rudi papo, panigedeme mgando

Ningaambwa kwetu hapo, kwamba kwanuka uvundo

Sitakwenda penginepo, tarudi kuko kwa mwando

Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini

  1. Naja sitapakimbiya, ningambwa kuna vimondo

‘Takuja kuvilekeya, vinganijiya kwa vundo

nilipozawa tafiya, sikimbii kwenda kando

nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini

  1. Naja hiwa ‘mekomaa, kuzidi nilivyo mwando

Tena n’najiandaa, kwa fikira na vitendo

Kwetu nije kuifaa, na kuitiliya pondo

Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini

  1. Naja na ingawa naja, siwaeki mifundo

Moyo wangu ushatuja, mawi nalotendwa mwando

Ela wataoningoja, na vyao viwi vitendo

Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini

7.    a)  Eleza jinsi ‘uzalendo’ wa mshairi unavyojitokeza katika beti za 1 na 2        alama 4

  • Fafanua jazanda zinazopatikana katika mshororo:

Kaa kwingine anapi, ela kwenye lakwe gando?                                             alama 2

  • Andika ubeti wa tatu katika lugha nathari                                                      alama 4
  • (i)   Katika ubeti wa 5 mshairi amebadilika Eleza                                         alama 2

(ii)   Ananuia kufanya nini pindi arudipo?                                                     Alama 2

  • Eleza ujumbe unaopatikana katika ubeti wa 6                                               alama  2
  • Andika maneno haya katika kiswahili sanifu                                                 alama  2
    • Mwando
    • Ningambwa
  • Kibwagizo cha shairi kinampa sifa gani mshairi?                                          Alama 2

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA SHAIRI WA 1

7)   `UZalendo’

(i)   Anarudi kwao

(ii)  Anapenda kwao

(iii)Anatamani kwao

(iv) Nyumbani kunamlisha

(v) Ndiko kuna uhondo

(vi) Hawezi kulinganisha kwao na kwingine                                                             zozote 4 x 1 4

b) Jazanda

(i)   Anajilinganisha na kaa na angeishi baharini mahali pakubwa

(ii)Kaa ana lile gando, kile kifaa anachokitumia kupatia chakula na vile vile kama silabi, paini nyumba ambapo pana chakula na usalama au mtu kwao ni kwao ndipo pampapo riziki/  ussalama na utulivu

                                                                                                                                    2×1 = 2

c) Lugha Nathari

(i)    Ninarudi  hapo kwetu

(ii) Hata nikiambiwa pananuka

(iii)  Siendi pengine narudi hapo tu

(iv)  Nyundo/ Mjuzi/ Bingwa/ Shujaa/ Mweledi/ Stadi ninakuja misumar jihadhari alama 4 x 1 = 4

d)  (i)  Amekomaa zaidi anajiandaa kwa fikira na vitendo                                                    alama 2

     (ii) Kuifaa nchi yake kuleta maendeleo /kurekebisha kujenga mji/ kuondoa uhasama    alama 2

e.  (i)   Yeye hana kinyongo anapokuja (lakini kwa waliomtenda na wale wanaomngojea kwa maovu atapambana nao)                                                                                                                     alama 2

f) (i)  Mwando – Mwanzo

    (ii) Ningambwa – Ningeambiwa                                                                                        2×1 =2

g)   sifa inayopatikana katika shairi kuhusu mhusika

            (i)  hajabadilika (ni ile nyundo / bado yu tayari)

            (ii) bado yu tayari kupambana na matatizo na anaweza/ mtekelezi                           2 x 1 = 2

USHAIRI WA 2

Soma shairi hili kisha ujibu maswali.

Jukwani naingia, huku hapa pasokota,

Kwa uchungu ninalia,hii tumbo nitaikata,

Msiba mejiletea,nimekila kiso takata,

We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

Wazee hata vijana,wote umewasubua,

Huruma nao hauna,heshima kawakosea,

Ukambani na Sagana,hata mbwa wararua,

We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

Wahasibu ofisini,kibwebwe mejifunga,

Miaka mingi vitabuni,ili wasikose unga,

Nadhari wanadhamini,hesabu wanazirenga,

We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Wapenzi wa kiholela,pia wanakuogopa,

Baada yao kulala, wana wao wanatupa,

Wakihitaji chakula,wanachokora mapipa,

We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

Wafugaji hata nao,kama dawa wakwamini,

Hawajali jiranio,wamesusia amani,

Wanaiba ng’ombe wao,na kuzua kisirani,

We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

Nayo mizozo ya maji, kaonekana kwa mara,

Hiyo nayo ni dibaji,sababu sio harara,

Njaa wahepe wenyeji, huo ndio mkarara,

We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

Ningeweza kukuuza,ingekuwa siku njema,

Tena kwa bei ya meza,sokoni nimesimama,

Wala tena singewaza,kuhusu wali na sima,

We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

Hatima umefikika,naenda zangu nikale,

Mate yanidondoka,kwa mnukio wa wale,

Naomba kwenda kukaa,wala sio nikalale,

We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

Maswali

  1. Lipe anwani mwafaka shairi hili.                                                                                     (Alama 2)
  2. Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.                                                                               (Alama 2)
  3. Huku ukitolea mifano mwafaka, taja arudhi zilizotumiwa katika ubeti wa tatu.                (Alama 4)
  4. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari.                                                                           (Alama 4)
  5. Thibitisha kuwepo kwa idhini ya ushairi.                                                                         (Alama 2)
  6. Taja madhila anayoelezea mtunzi wa shairi hili yaletwayo na tumbo.                                (Alama 4)
  7. Elezea maana ya maneno yafuatayo.                                                                                 (Alama 2)

(a) Dibaji

(b) Harara

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 2

1.        

            i)          –           Tumbo lisilotosheka

                        –           Matatizo ya tumbo                                                                                          2×1=2

            ii)         –           Tarbia- mishororo minne                                                                                2×1=2

            iii)        –           Mishororo

  • Vina vya kati (ni) na vya mwisho (nga)
  • Vipande viwili- utao na ukwapi
  • Kibwagizo
  • Mizani (urari wa mizani ukwapi 8 na utao 8) jumla 16                                 4×1=4

iv)        –           Wapendanao mapenzi yasiyo na dhati wanakuogopa. Wapatao mimba, watoto wao hawajali. Watoto watakapo chakula huwa wanatafuta mapipani. Tumbo nikupe nini ili utosheke?

                                                                                                                                                4×1=4

v)         –           Kukosa heshima- hata mbwa wararua

            –           Ufisadi- hesabu wanazirenga

            –           Kutowajibikia wana- wanachokora mapipa

            –           wizi- wa ng’ombe

            –           Mizozo/ kutoelewana- mradi waliepe njaa                                                     4×1=4

vi)        –           Dibaji- Thibitisho/ uhalali

                        Harara- hasira/ hamaki                                                                                    2×1=2

USHAIRIWA 3

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

  LAU HAKUNA MAUTI. Na Abdalla Said Kizere

  1. Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,

Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,

Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

  • Dunia ingetatana, na kizazi katikati,

Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti,

Vipi tungelioana, na kuzaa hatuwati?

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

  • Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti,

Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati,

Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati?

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

  • Walakini Subuhana, kapanga sisi na miti,

Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti

Maisha ya kupishana, yule ende yule keti,

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

  • Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti,

Kwa uwezowe Rabana, kaipanga madhubuti,

Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti,

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

  • Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati,

Sote tungeambatana, kama ukosi na shati,

Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati,

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

  • Peleleza utaona, hayataki utafiti,

Kama tungelikongana, ingekuwa ni bahati,

Vipi tungesukumana, katika hiyo hayati?

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

  • Mbele sitokwenda tena, hapa mwisho nasukuti,

Yaoleni waungwana, shauri yake Jabaruti,

Yote tuloelezana, katenda bila senti,

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

MASWALI

a)  Je, hili ni shairi la bahari gani? Eleza                                            (alama 2)

b)   Eleza vile mwandishi alivyotumia uhuru wa kishairi                   (alama 4)

c)   Eleza umbo la shairi hili                                                               (alama 4)

d)  Fafanua ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano                      (alama 4)

e)  Andika majina mawili ya Mungu kwa mujibu wa shairi               (alama 2)

f)  Kwa kutolea mifano, eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili                                                                                                             (alama 2)

g)  Eleza maana ya maneno yafuatayo kulingana na shairi                (alama 2)

                        (i)   Tiati _________________

                        (ii)  Shani_________________

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 3

  1. (i)  Tarbia – – mishororo mine

(ii) Pindu  – utao katika mkarara ndio kianzio cha ubeti unaofuatia mf. Ubeti 3

iii) Mtiririko – vina vya kati vinafanana na vya mwisho pia vinafanana katika shairi lote

Vya kati                            vya mwisho

 na,                                                ti,

 na,                                                ti,

na,                                                 ti,

ti,                                                   na.

(iv)  mathnawi – lina vipande viwili – utao na ukwapi

b)  (i)         Inkisari –kwazawa, ńgekuwa, ńgetutafuna, nanena, sitokwenda

  •   Tabdila – Sharuti badala ya sharti
  • Kuboronga sarufi – mauti kawa hakuna – ikiwa hakuna mauti,

                             – katika wote wakati  – katika wakati wote

  • Lahaja (ya kimvita)  – hatuwati (hatuwachi)
  •                                   – yaoleni (yaoneni)

c) 

  • Beti 8
  • Mishororo 4 katika kila ubeti
  • mizani 16 katika kila mshororo
  • vina vya kati                      vya mwisho

na,                                     ti,

na,                                     ti,

na,                                     ti,

ti,                                       na.

  • vipande viwili – utao na ukwapi
  • Lina kibwagizo kinarudiwarudiwa “lau hakuna mauti, vipi tungelisongeni

d)  (i)   Dunia haiwezi kujaa watu kupita kiasi

     (ii)   Mwenyezi Mungu anajua kupanga

  • Baadhi ya watu wafe na baadhi wazaliwe
  • Bila kifo tungesongamana/jaa sana                                             

e)   (i)   Subuhana

      (ii)   Rabana

      (iii)   Jabaruti                                                                    

f)  (i)   Balagha – k.v  Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?

    (ii)   Tashbihi   – ikawa kama ya kuti

  • Kama ukosi na shati

    (iii)   Takriri   – si ati ati

  • Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?   

USHAIRI WA 4

Soma shairi  lifuatalo, kisha ujibu maswali;                                              (alama 20)

Sinisumbuwe akili, nakusihi e mwendani,

Afiya yangu dhahili, mno nataka amani,

Nawe umenikabili, nenende sipitalini,

Sisi tokea azali, twenda zetu mizimuni,

Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Mababu hawakujali, wajihisipo tabani,

Tuna dawa za asili, hupati sipitalini,

Kwa nguvu za kirijali, mkuyati uamini,

Kaafuri pia kali, dawa ya ndwele Fulani,

Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Mtu akiwa halali, tumbo lina walakini,

Dawa yake ni subili, au zongo huauni,

Zabadi pia sahali, kwa maradhi yalondani,

Au kwenda wasaili, wenyewe walo pangani,

Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Mtu kwenda sipitali, ni kutojuwa yakini,

Dakitari k’ona mwili, tanena kensa tumboni,

Visu vitiwe makali, tayari kwa pirisheni,

Ukatwe kama figili, tumbo nyangwe na maini,

Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Japo maradhi dhahili, kuteguliwa tegoni,

Yakifika sipitali, huwa hayana kifani,

Wambiwa damu kalili, ndugu msaidieni,

Watu wakitaamali, kumbe ndiyo buriani,

Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

Mizimu wakupa kweli, wakueleze undani,

Maradhiyo ni ajali, yataka vitu thamani,

Ulete kuku wawili, wa manjano na kijani,

Matunda pia asali, vitu vyae chanoni,

Nafwatani sipitali, na dawa zi mlangoni?

MASWALI – USHAIRI                                                                               (ALAMA 20)

a)  Lipe kichwa mwafaka shairi hili.                                                                           (alama 2)

b)  Mtunzi alikuwa na lengo gani alipotunga shairi hili?                                           (alama 2)

c)  Mbona mshairi hataki kwenda hospitali?                                                              (alama 4)

d)  Kwa kuzingatia muundo wa shairi hili, eleza mbinu zilizotumika                        (alama 6)

e)  kwa nini mshairi alitumia ritifaa katika ushairi?                                                   (alama 2)

f)  Andika maana ya maneno yafuatayo yalivyotumika katika shairi                 (alama 4)

i)  Dhahili

ii)  Azali

iii) Sahali

iv)  Tumbo nyangwe

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI 4

            a)         i)          Sipitali sendi/ siendi

                        ii)         Udhaifu wa hospitali

                        iii)        Umaarufu wa miti- shamba                                       

            b)         i)          Kupigia debe miti- shamba

                        ii)         Kukosoa huduma za hospitali                                                            

            c)         i)          Tangu zamani, wao huenda mzimuni

                        ii)         Madawa ya asili yapo

                        iii)        Hapendi upasuaji

  1. Mtu anaweza kupoteza maisha
  2. Tunafuata kieleleza cha mababu wetu                                              

d)         i)          Inkisani- tabani, wambiwa

            ii)         Mazida- Afiya

  1. Takhmisa- Mishororo tano
  2. Kibwagizo- Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?
  3. Mtiririko (vina vya kati ni “li” ilhali vya utao ni “ni”
  4. Mizani kumi na sita kwa kila mshororo                     

e)         Inkinsani                                                                                                                    

f)         i)          Dhalili- Hafifu, isio na nguvu

            ii)         Azali- zamani

  1. Sahali- Nafuu

Tumbo nyangwe- Utumbo mdogo 

USHAIRI WA 5

1.         Soma shairi lifuatalo kwa makini kisha ujibu maswali.

Niokoa Muokozi, uniondolee mashaka.

Kuyatukua siwezi, mjayo nimedhikika

Nimekithiri simanzi, ni katika kuudhika

Mja wako nasumbuka, nipate niyatakayo.

Mja wako nasumbuka, nataka kwao afua

Nirehemu kwa haraka, nami nipate pumua

Naomba hisikitika, na mikono hiinua

Mtenda ndiwe Moliwa, nipate niyatakayo.

Mtenda ndiwe Moliwa, we ndiwe Mola wa anga

Mazito kuyaondoa, pamoja na kuyatenga

Ukauepusha ukiwa, ya pingu zilonifunga

Nikundulia  muwanga, nipate niyatakayo

Muwanga nikundulia, nipate toka kizani

Na huzuni n’ondolea, itoke mwangu moyoni

Mambo mema niegheshea, maovu nisitamani.

Nitendea we Manani, nipate niyatakayo.      

Igeuze  yangu nia, dhaifu unipe mema

Nili katika dunia, kwa afia na uzima

Moliwa nitimizia, yatimize yawe mema

Nifurahike mtima, nipate niyatakayo.

  • Shairi hili ni la bahari gani? Eleza.                                                           (alama 2)
  • Taja madhumuni  ya shairi hili.                                                                (alama 3)

(c) Eleza muundo wa shairi hili.                                                                     (alama 4)

(d) Thibitisha namna uhuru wa kishairi unaibuka katika shairi.                     (alama 4)

(e) Andika ubeti wa pili katika lugha sufufu.                                                 (alama 4)

(f) Toa maana ya:

  • Nimedhikika
  • Muwanga nikundulia
  • Nifurahike mtima                                                                                (alama 3)

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 5

1.         a)         Pindu- Kifungu katika mshororo wa mwisho wa ubeti kuanza ubeti mpya               1×2=2

b)         –Kuonyesha kuwa mja hana nguvu

-Amekumbwa na masaibu

-Maombi kwa mola amwokoe na ampe afya

-Mungu amtoe katika giza

-Mungu ampe maisha mema

                                                                                                                                     Zozote 3×1=3 mks

c)         Muundo

                        -Tarbia

                        -Vina vya kati na vya mwisho

                        -Mizani

                        -Kibwagizo

                                                                                                                                                4×1=4 mks

d)         Inksari-

                        -Mjayo; Mja waho

                        -Nondolea

                        -Zilonifunga

Mazida –Moliwa

Tabdila –Afia

Kuboronga sarufi –igeuze yangu nia

                                                                                                                                                4×1=4mks

e)         Kiumbe wako nimeteseka mno. Naomba unipe afueni na unirehemu. Ninaomba nikikusudia. Wewe ndiwe Muumba unayeweza kunipa niyahitajiyo.                                4×1=4mks

f) i)      Nimeteseka au ni taabani

   ii)      Nimulikie; niletee nuru, nizinduke

  iii)     Nichangamke au nistarehe moyoni.

   

Scroll to Top