Please Limited time Offer!

Mbinu za Sanaa katika Riwaya ya Chozi la Heri

UNUKUZI KUTOKA BIBLIA.

Hii ni mbinu ya kunukuu visa tofauti kutoka kwenye Biblia. Assumpta K.Matlei amejikita sana katika mbinu hii ya kunukuu

Biblia, kama tunavyoona kutokana na mifano ifuatayo.

Katika ukurasa wa 36; “Aliweza kuudhibiti ugonjwa wa shinikizo la damu ambao ulitokana na mshtuko wa kupoteza jamaa na mali yake dafrao moja. Awali akijihisi kama yule Ayubu kwenye kitabu kitakatifu ambaye ibilisi aliifakamia familia na mali yake takriban kutwa moja”

Katika ukurasa wa 46; “Umbali ulio kati yao, japo ni hatua tatu tu, waonekana kama upana wa bahari ya Shamu wakati Waisraeli walipokuwa wakikamia wokovu wao kutokana na dhuluma ya wamisri “

Katika ukurasa wa 47; “Walishikana kukutu, kila mmoja akimwambia mwenzake kimoyomoyo, “Ni hai Sijafa “Ikawa ni kama Yesu anamhakikishia “Tomaso asiyeamini”,”Tazama hii mikono yangu. Nipe mkono wako, utie ubavuni mwangu. Usikose kuamini tena.

Katika ukurasa wa 34; “Baada ya kuishi kwenye msitu wa Mamba kwa miezi sita, Ridhaa, Kaizari na familia yake walibahatika kurudi nyumbani kufuatia mradi ulioitwa na wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu Operesheni Rudi Edeni “

KEJELI.

Hii ni mbinu ya Sanaa inayotumia maneno kudharau au kukemea kitendo au mtu fulani. Mwandishi pia anatumia mbinu hii kuwasilisha maudhui yake kwenye kazi yake ya kifasihi.

Katika ukurasa wa 15; “Kuna wale ambao hufia kwenye vitanda vyao vya mwakisu vitongojini baada ya kupiga haramu. Hawa husemekana kuwa wamekuwa nzi ambao kufia dondani si hasara. Hulaumiwa kwa kujitosa katika msiba wa kujitakia “Hawa watua mabao wanakunywa pombe haramu na kufia kwao nyumbani ambako kumekithiri ukata, wanadharauliwa na kulinganishwa na huyo nzi afaye kwenye donda, kwani wanafanya jambo kwa hiari yao, huku wakijua madhara na matokeo yake ni yepi.

NJOZI AU NDOTO.

Mwandishi hutumia njozi au ndoto kutabiri jambo litakalofanyika au kufumbua jambo lililokuwa limefumbwa.

Katika ukurasa wa 2; “Anakumbuka akimwambia mkewe Terry, “Milio hii ni kama mbiu ya mgambo, huenda kukawa na jambo “Terry kwa ucheshi wake wa kawaida hakunyamaza “

“Ridhaa akamwambia, “wewe endelea kupiga hulu tu, lakini utakuja kuniambia”

Ridhaa alikuwa na ndoto ya kuwa kuna jambo mbaya au lisilo la kupendeza ambalo lingeweza kutendeka, na kwa kweli, njozi lake likawa ni la ukkweli wakati lilipo timia.

KISENGERE MBELE.

Hii ni mbinu ambayo mwandishi hutumia katika Sanaa yake.

Inahusisha mwandishi kubadilisha wakati na kusimulia mambo yatakavyokuwa siku za usoni; au kutumia isiyo moja kwa moja kutabiri yatakayojiri.

Mbinu hii pia huitwa utabiri.

Katika ukurasa wa 45;”Sasa anapotazama nyuma anaona kuwa ule utabiri wa ‘wingu la mabadiliko’ wa mwalimu ulikuja

Kutumia “Ni kweli mwalimu alikuwa ametabiri kuhusu wingu hili Ia mabadiliko ambalo kwa sasa limetanda (uk 44)

Tila: Ambayo mshahara wake ni mkia wa mbuzi.Baba, kile ambacho raiyaa wanahitaji ni mabadiliko ya mara kwa mara ya uongozi na sera zenyewe za uongozi Na naona awamu hii, kama asemavyo mwalimu, wingu la mabadiliko limetanda.

Katika ukurasa wa 70;Lunga alikuwa ameona kuwa maisha yake yalikuwa yakielekea kudidimia hata kabla ya kuhamia makao hayo yake mapya ambayo anadai kuwa jaala kampeleka huko “Ametononeka si haba katika msitu huu. Hadiriki kuwaza kwamba msitu huu unastahili kuhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye Kabla ya jaala kumleta hapa, lunga aliuona mstakabali wa maisha yake ukiporomoka. Alikuwa ameipoteza kazi yake “

MAZUNGUMZO.

Haya ni majailiano ya jambo Fulani baina ya watu wawili au Zaidi. Kila mtu huzungumza kwa wakati wake, na kumpa mwingine nafasi ya kusikiliza.

Uk 38;”Tila:Shikamoo baba.

Ridhaa:Marahaba mwanangu. Umeshindaje?

Tila:(kwa uchangamfu)vyema. Baba, leo somo letu la fasihi lilivutia mno.

Ridhaa:Kwani waliwafunza nini huko?Ama ni zile siasa zenu zisizoisha?Leo mwalimu Meli alitueleza jinsi mifumo ya uzai

Tila:ishaji mmali ilivyobadilika, kuanzia wakati wa ujima,ukabila, ubwanyenye, ujamaa hadi sasa tunapopambana na utandawazi. Lakini anasema ujamaa si rahisi kutekelezwa.

Ridhaa: (kwa wasiwasi) Kipi kiini hasa cha kufunza mada hii kwa watoto wakembe kama nyinyi?siku zetu sikumbuki kuona mada hii hata katika mtalaa wa kidato cha sita Nadhani umesahau baba. Suala hili ulisema limeshu

Tila:ghulikiwa katika kazi za kifasihi kama vile Mashetani,ile tamthilia ya Hussein inayoisawiri migogoro ya kisiasa, kiuchUmi na kijamii ya baada ya ukoloni lsitoshe, mwalimu alitaka tu kuonyesha kwamba upo uhusiano kati ya mfumo wa kiuchu na rmurnv wa Kislasa alituambia kwamba mfumo wa kiuchumi hudhibitiana na mfumo wa kisiasa. Utawala huteuliwa makusUdi kuendeleza mfumo uliopo wa kiuchumi kwa maslaya watawala na tabaka ambalo linazimiliki nyenzo za uzalishaji mmali.(kama aliyeudhika).Naona mmeanza kuingjlia

Ridhaa:Nyanja ambazo ni michezo yaw engine na wanafaa kuachiwa wao.Lakini baba, unajua hatuwezi kuyafumbia macho

Tila:mabadiliko yanayozikumba jamii zetu kwa mfano,kura ya maoni ya hivi maajuzi yaonyesha kwamba majimbo mengi nchini yanamuunga mkono Bi.Mwekevu Tendakazi. Ameongoza kwa asilimia sitini. Mpinzani wake wa karibu wa kiume ana asilimia thelahini. Mwalimu alisema kuwa wakati umefika kwa jamii kuacha kuacha kupima uwajibikaji wa mtu kwa misingi ya kijinsia. Wote waume kwa wake wapewe nafasi sawa.Si kwamaba napinga hili. Ningekuwa hasidi wa

Ridhaa:usawa wa kijinsia nisingewapelekeni nyinyi shuleni.Ningemshughulikia Mwangeka tu ambaye jamii inaamini kuwa nndiye mridhi wa mali yangu.Hata hivyo, naona kwamba ni mapema mno kuanza kulitolea hukumu suala la nani anaongoza. Huku kutakuwa kukata mbeleko kabla ya mtoto kuzaliwa.(akichekacheka)DaliIi ya mvua ni mawingu baba. Mara hii kama wapiga kura tumeamua kujaribu mbinju mpya za kilimo. Haya matumzi ya visagalimma yarneanza kupitwa na wakati.

Ridhaa: Tila Kummbuka hapo ulipo hata kura yenyewe hauna Naona wamekutia maneno ya uchokozi. Ngojea kipindi kingine cha uchaguzi kifike,utakuwa na haki ya kuchukua kura na kumpigia mwanamke umtakaye. Kwa sasa itabidi utosheke na chaguo letu

Tila: Lakini baba, sijasema tunataka kipongozi mwanamke. Sisi tunataka kiongozi yeyote awe mwanamke au mwamume, atakayeweza kulielekeza jahazi hili letu kwenye visiwa vya hazina. Tufikie kilele cha maendeleo pale tutakapofikia malengo ya nkimaenndeleo ya kimilenia. Kiongozi ambaye ataendeleza Zaidi juhudi za kukabiliana na na wale maadui ambao wewe daima huniambii kuhusu: umaskini, ujinga, magonjw (akisita kumtazama baba) uhaba wa nafasi za kazi na ufuisadi. Je, huu sio uliokuwa muono wa waliopigania uhuru?siyo ambayo viongozi waliochukua hatamu za uongozi kutoka kwa watu weupe waliyofanya juu chini kutekeleza?

Ridhaa:Na nani akasema viongozi waliopo hawajajikuna wajipatapo?Huoni hata wahasiriwa wa magonjwa sugu kama vile iri na hata UKIMWI wana dawa za bei nafuu za kuwawezesha kudhibiti hali hizi?Je, serikali haijaanzisha sera ya elimu bila malipo kwa Shule zote za msingi?Haijagharamia karo za Shule za kutwa katika Shule za upili?kumbuka pia na ule mradi wa kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi kuanzia darasa la kwanza ana kipakatalishi chake?Ushaona?Hivi karibuni, nchi Inafikia ile vision 2030 hata kabla ya 2030 yenyewe  Je, ni tume ngapi za kuchunguza kashfa za kifisadi ambazo zimeundwa?Hizo si juhudi za kupigana na ufisadi?Serikali imetumia bilioni ngapi katika shughuli ya kuhesabiwa kwa watu mwaka jana?Unajua sababu ya shughuli hiiTvoiongozi wanataka kupata takwimu sahihi Zaidi na za kutegemewa, zitakazowawezesha viongozi kujua mahitaji ya kiuchumi na ya kijamii ya kila jimbo. Huduma zitaweza kutolewa kwa urahisi Zaidi katika kila eneoo la ugatuzi.

Tila: Na umaskini, je, baba?Mara nyingi hukuona umejishika tama ukilalamikia asilimia kubwa ya raia ambao hawamudu hata gharama ya matibabu ya kimsingi si wewe unayesema kwamba vifo vingi vya watoto chini ya miaka mitano husababishwa na magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora, pamoja na wazazi na walezi kutopata elimu kuhusu njia za kujikinga dhidi ya baadhi ya magonjwa?

Ridhaa: (kwa msisitizo)Kumbuka kwamba haya malengo ya kimilenia hayajaanza kupigiwa Shabaha sasa. Kilichobadilika ni istilali ya kuyarejelea jawapo ya haki za kibinadamu ambazo wanaharakati mapinduzi walipigania ni matibabu boila malipo kwa wasiojiweza kiuchumi, na elimu ya lazima, na bila malipo kwa watoto wote, kufikia umri wa miaka kumi na mitano. Na nadhani kile ambacho mmwalimu wenu angewasisitizia Zaidi ni kwamba vijana wana jukumu la kuelimishana kuhusu nafasi ya kila mmoja wao katika kuuboresha uongozi uliopo sasa. Watumie vipawa vyao kwa njia endelevu ili kusaidia katika kuzalisha nafasi za kazi badala ya kungojea serikali iwatilie riziki vinywani. Nchi haijjengwi kwa mihemko na papara za ujana. Na suala la umaskini?Naona hili ni tatizo la kijaamii. Mathalan, watu wanaoishi katika sehemu kame wanastahili kujitahidi kuvumbua mbinu za kuyahifahi maji ya mvua. Pia kila eneo la ugatuzi halina budi kuwashajiisha wataalamu wake kujizika katika uafiti ili kuvumbua rasilimali zinazopatiakana katika maeneo haya, hili litawawezesha maeneo yenyewe kuzitumia raslimali kwa njia endelevu. Haya yote yatasaidia kupunguz mng’ato wa uhawinde.

Tila: Watayahifadhi vipi maji haya kama mvua yenyewe hainyeshi?Baba, wewe mwenyewe unalalamika kiangazi ambacho kimmezikumba sehemu mbalimbali nchini isitoshe, mwalimu asema kwamba asilimia kubwa ya wakazi wa sehemu kame haiwezi hata kumudu kula mara mbili kwa siku. Hizo hela za kununulia matangi ya kuhifadhia maji na kufanyia utafiti watazitoa wapi?

Ridhaa: Basi watumie maji ya mabombalSi lazima wahifadhi ya mvualNa huyo mwalimu naona anapanda mbegu za uhasama kati ya viongozi na vijana. Vijana hawapaswi kungojea kufanyiwa kila kitu. Tumewapa nyavu za kuvulia, nao wanaona wangoje kuletewa samaki

Tila: (akionyesha kuvunjika moyo)Baba!Umekuwa kama yule kiongozi wa kifaransa, unayeniambia wewe kila mara, ambaye alipoambiwa kuwa wanyonge hawakuwa na mkate alisema, “if there is no bread, let them eat cake” Watu wengi huko mashambani hutegemea mashamba, mvua haijakubali kunyesha kwa muda. Wengi wa wanaofanya kazi za ajira, hufanya kazi za kijungujiko. Sasa mabomba yatatoka wapi?na hata kama mabomba yenyewe yangekuwepo, juzi nimeskia kwenye runinga kwamba bwawa la Fanisi ambalo ndilo lililotegemewa sana kutoa maji kwenye sehemu kame halitasambaza maji tena kwa sababu kiwango cha maji kimeshuka sana. Mabomba yenyewe yamejikaukia

Ridhaa: Serikali imeanzisha mpango wa kusambaza huduma za maji na umeme katika sehemu za mashambani, hususan zile kame. Wanachohitaji ni subira tu. Na nadhani mwalimu wenu alisahau kuwaambia kuwa katika baadhi ya sehemu mna machimbo ya mawe ya ujenzi, vito, na hazina za mamfuta. Wenyeji wana jukumu la kutumia raslimali hizi kujiendeleza.

Tila: Alituambia hayo pia. Lakini kuna tayari kampuni za kibinafsi ambazo zimetumwa huko kuchimbua madini haya. Isitoshe, kampuni zilioshinda zabuni za kuyachimbua madini haya ni za kigeni. Uchimbaji wenyewe unafadhiliwa na wawekezaji wa kigeni.Raiya watafaidika vipi?Fedha zinazotokana na raslimali hii yahofiwa kuwa zitaishia kwenye mifuko ya wageni. Zinatumwa kuendeleza nchi za hao hao wawekezaji wanaodaiwa kuwa wawekezaji.

Ridhaa: Ni kweli lakini kumbuka kuwa kampuni hizi zimebuni nafasi za kazi. Wenyeji wamepata ajira

Tila: Ambayo mshahara wake ni mkia wa mbuzi. Baba, kile ambacho raiyaa wanahitaji ni mabadiliko ya mara kwa mara ya uongozi na sera zenyewe za uongozilNa naona awamu hii, kama asemavyo mwalimu, wingu la mabadiliko limetanda.

Scroll to Top