SEHEMU YA A: TAMTHILIA
KCSE 2022 Prediction Kiswahili Pp3 P. Kea: Kigogo
- Lazima
(a)Jadili jinsi kumi ambazo maudhui ya ukatili yanajitokeza katika Tamthilia ya Kigogo (alama 10)
(b)Eleza mifano kumi ya matumizi ya kinaya katika Tamthilia ya Kigogo. (alama 10)
SEHEMU YA B
RIWAYA: CHOZI LA HERI
(Assumpta K. Matei)
Jibu swali la Pili au la Tatu
2. “Watu husema kuwa binadamu hawawi sawa ila kifoni…”
a) Eleza muktadha wa maneno haya. (alalama 4)
b) Tambua mbinu moja ya lugha iliyotumiwa katika dondoo hili. (alama 2)
c) Eleza sifa na umuhimu wa mzungumzaji wa maneno haya. (alama 6)
d) Thibitisha kuwa hakuna usawa baina ya wanadamu. (alama 8)
Au
3. Jadili nafasi ya sehemu zifuatazo katika riwaya ya Chozi la Hari:
(a) Hotuba (alama 10)
(b) Uozo katika jamii (alama 10)
KCSE 2022 Prediction Kiswahili Pp3 SEHEMU C: HADITHI FUPI
(Mtihani wa maisha)
‘Leo mwalimu mkuu atajua kwamba mdharao biu hubiuka’
(a)Eleza muktadha wa maneno haya. (Alama 4)
(b)Taja mbinu ya lugha iliyotumika katika mktadha huu. (Alama 6)
(c)Eleza wasifu wa mzungumzaji wa maneno haya. (Alama 2)
(d)Jadili maudhui ya elimu kama yanavyojitokeza katika hadithi hii. (Alama 8)
(Ndoto ya mashaka (Ali Abdulla)
(5) ’Kusema kweli lakini hata mimi sikuwa na nadhari katika kumpenda msichana huyu … Nilimpenda kufa! Lakini! Kwao bure tu!’
(a) Eleza mkutadha huu. (Alama 4)
(b)Taja mtindo wa lugha uliotumika katika mkutadha huu. Alama 4
(c) Taja sifa mbili za mzungumzaji. (Alama 2)
(d) Onyesha maudhui ya umaskini katika hadithi fupi ya Ndoto ya mashaka.
KCSE 2022 Prediction Kiswahili Pp3 SEHEMU YA D: USHAIRI
Jibu swali 6 au 7
(6) USHAIRI
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
Daima alfajiri namapema
Hunipitia na jembe na kotama
Katika njia iendayo kondeni
Kama walivyofanya babuze zamani; Nimuonapo huwa anatabasamu Kama mtu aliye na kubwa hamu Kushika mpini na kutokwa jasho Ili kujikimu kupata malisho.
Anapotembea anasikiliza Videge vya anga vinavyotumbuiza Utadhani huwa vimemngojea Kwa usiku kucha kuja kumwimbia; Pia pepo baridi kumpepea Rihi ya maua zikimletea Nao umande kumbusu miguu; Ni miti yote hujipinda migongo Kumpapasa, kumtoa matongo; Na yeye kuendelea kwa furaha Kuliko yeyote ninayemjua
Akichekelea ha ha ha ha ha ha ha … Na mimi kubaki kujiuliza Kuna siri gani inayomliwaza? Au ni kujua au kutojua? Furaha ya mtu ni furaha gani Katika dunia inayomhini? Ukali wa jua wamnyima zao Soko la dunia lamkaba koo; Dini za kudhani zamsonga roho Ayalimia matumbo ya waroho; Kuna jambo gani linamridhisha? Kama si kujua ni kutokujua Laiti angalijua, laiti angalijua!
(a)Eleza matatizo manne yanayompata mzungumziwa. (Alama 4)
(b)Eleza mtindo wa lugha uliotumiwa na mshairi na utoe mifano. (Alama 8)
(c)Taja nafsineni katika shairi hili. (Alama 1)
(d)Eleza toni ya shairi hili. (Alama 1 )
(e)Taja mbinu mbili za uhuru wa kishairi uliotumika na utoe mifano. ( Alama 2)
(f) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya nathari. (Alama 4)
(7)Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili
Vitisho pamwe kelele, ninavicha, kwa nafsi na mwili
Ila ugonjwa utimile, umechacha, na kuudhili mwili
Msikose simile, magalacha, si gurudumu mwili.
Vingekuwepop viraka, kuutia, ngeushuruti mwili
Kifundi kivipachika, kuingia, hata kuridhi mwili
Upya ukaungilika, kuvutia, roho na wake mwili.
Lakini kamwe haiwi, kuvipata, vipande vyake mwili Sihofu kupata mawi, sitajua, kupigania mwili
Hata kufutwa sikawi, nitakita, kidete nao mwili.
Kazi ninaithamini, ni hakika, akilini na mwili
Ila kamwe siamini, kusagika, damu, jasho na mwili
Uwele hususani, kioneka, nguvu hitishi mwili.
(a)Liweke shairi hili katika bahari tatu. (Alama 3)
(b)Eleza dhamira ya mshairi. (Alama 2)
(c) Eleza muundo wa shairi hili. (Alama 4)
(d) Toa mifano ya uhuru wa kishairi uliotumika. ( Alama 4)
(e)Eleza kwa kifupi maudhui matatu yanayojitokeza katika shairi hili. (Alama 3)
(f) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya nathari. (Alama 4)
KCSE 2022 Prediction Kiswahili Pp3 SEHEMU D: FASIHI SIMULIZI
A(i) Miviga ni nini? (Alama 2)
(ii) Eleza sifa nane za miviga. (Alama 8)
B (i) Ulumbi ni nini? (Alama 2)
(ii)Eleza sifa nane za ulumbi (Alama 8)