Please Limited time Offer!

KCSE Prediction Kiswahili pp1 Marking schemes

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

KISWAHILI 102/1

1.         Swali la kwanza.

   (i)     Hii ni barua rasmi kwa mhariri.

   (ii)    Utaratibu wa kuandika barua rasmi lazima uzingatiwe.

            Baadhi ya sehemu muhimu za kuzingatiwa ni:-

  (a)      Anwani mbili.

              (b)     Kichwa / mada yaani Mint / Ku / Reje.

              (c)      Kianzio cha salamu kwa mfano kwa mhariri.

              (d)     Mwili ambapo hoja za sababu za ajira za watoto zitajadiliwa.

              (e)      Hitimisho ambapo anaweza kutoa mwito, matumaini, changamoto na

                        kadhalika.

              (f)      Jina kamili la mwandishi na sahihi ziandikwe baada ya hitimisho.

(iii)      Baadhi ya hoja zinazotarajiwa ni:

             (a)       Umaskini unaowafanya wengi kukosa mahitaji ya kimsingi.

             (b)      Uyatima – Kufiwa na wazazi na kuwaacha bila wa kuwategemea.

             (c)       Mazingira magumu shuleni ambayo hupelekea wao kuacha shule na

                        kujiunga na ajira.

Kwa mfano: adhabu kali.

            (d)       Shinikizo la rika kuwashawishi wajiunge na ajira za mapema.

            (e)        Matumizi ya dawa za kulevya huchochea mahitaji ya ununuzi wa dawa

hizi.

            (f)        Kushawishiwa na waajiri kwa kuwa ajira ya watoto si ghali.

            (g)       Ufisadi – Viongozi kukosa kuwachukulia hatua wanaoendeleza ajira ya

watoto.

            (h)       Changamoto kama za shule kuwa mbali huwavunja moyo wa kuendelea

na masomo.

            (i)        Wazazi wasiojiweza (vilema) huwatuma watoto wao kufanya kazi.

            (j)         Hali ambapo watoto hawawezi kulalamikia hali zao huwafanya waajiri

kuwapendelea.

            (k)       Wazazi kuwalazimisha wana wao kufanya kazi za nyumbani.

                                                                                    Na hoja zingine zozote.

            TANBIHI.

Mtahiniwa atakayekosa kuwa na anwani mbili, aondolewa alama 4S baada ya kutuzwa.

SWALI LA PILI.

Ni insha ya ufafanuzi ambapo mtahiniwa lazima akubaliane na kauli aliyopewa, yaani vipakatalishi vimeleta manufaa mengi.

Maudhui.

Baadhi ya hoja za kuzingatiwa ni:-

   (i)     Mtu huweza kufanyia kazi yake popote atakako kwani inabebeka kwa urahisi.

   (ii)    Vinaweza kutumika nyumbani bila umeme kwani vina hifadhi ya umeme kwa muda.

   (iii)   Ni rahisi kusoma barua pepe kwa haraka.

      (iv)            Vina matumizi mengi sana kwa mfano kikotoo, kalenda, runinga n.k

      (v) Ni rahisi kubebeka katika mikutano.

     (vi) Vinarahisisha kazi ya watu wengi.

    (vii) Vimerahisisha masomo hasa katika kuandika makala marefu.

Tanbihi.

(a)        Atakayezingatia hasara, atakuwa amepungukiwa kimaudhui. Asipite kiwango cha

D (wastani)

            (b)       Insha bora ni ile iliyo na hoja 5 na zaidi zilizofafanuliwa vyema.

SWALI LA TATU.

   (a)     Hii ni insha ya methali ambapo lazima kisa kithibitishe ukweli na methali.

   (b)    Methali hii inamaanisha kuwa Achekaye kilema au mtu yeyote aliye na tatatizo naye itafika wakati wake wa kupatwa na janga kama hilo.

                        Matumizi.

     –      Hutumika kutahadharisha wale wanaowacheka wenzao wanapokuwa na matatizo ya kwamba wakati  wao utafika.

–           Kisa  kionyeshe hali ambapo mtu alisherekea wakati mwenzake alikuwa na shida naye baadaye apate shida.

Kisa kinaweza kudhihirisha hali zifuatazo:

      (a)  Mtu asherehekee mwenzake aliyefiwa naye baadaye afiliwe.

      (b) Mwanafunzi amcheke mwenzake asiyefaulu katika masomo naye baadaye asifaulu katika

mitihani.

      (c)  Tajiri amcheke maskini naye mali yake ipotee baadaye.

      (d) Kiongozi awacheke au awadharau anaowatawala baadaye uongozi umtoke.

      (e)  Mtu mzima amdhihaki mgonjwa naye apate magonjwa baadaye.

            Tanbihi.

      1.   Lazima kisa kidhihirishe pande mbili za methali.

            (i) Kucheka kilema.

            (ii) Kilema kumpata.

            Atakayezingatia upande mmoja tu atakuwa na upungufu wa maudhui na asipate kiwango

cha C.

Atakayetunga visa vingi lakini vithimbitishe ukweli wa methali ana upungufu wa kimtindo asipite kiwango cha C.

3.         Atakayekosa kutunga kisa yaani atumie mifano tu achukuliwe kuwa amepotokwa kimaudhui na awekwe katika kiwango cha D 03/20.

SWALI LA NNE.

    –       Hii ni insha ya mdokezo ambapo lazima kisa kianze kwa mdokezo aliopewa.

    –       Kisa chake lazima kilingane na mdokezo huu yawezekana kuna uvamizi uliotokea.

    –       Kisa kiafiki hali hii ambapo anaweza kuturejesha nyuma, akaeleza uvamizi ulivyotokea

Au  Aendelee tu na usimulizi na kueleza yaliyofuatia baadaye.

   –        Hali hii inaweza kuwa;

            (i) Kutekwa nyara.

            (ii) Kuvamiwa na majambazi nyumbani.

Tanbini:

            Endapo hataanza kwa mdokezo amepungukiwa kimtindo.

Muhimu.

1.         Insha zote lazima zitimize urefu unaokusudiwa.  Upungufu wowote

utashughulikiwa kulingana na mwongozo wa kudumu.

2.         Insha zote (2, 3 na 4) lazima ziwe na vichwa.  Mtahiniwa akiacha kichwa

achukuliwe kuwa amepungukiwa kimtindo.

3.         Mtahiniwa lazima asome kwa makini mtungo wa mtahiniwa akizingatia mada na matumizi ya miongozo miwili yaani wa maswali wa na viwango ili kuiweka insha ya mwanafunzi katika kiwango chake.

MWONGOZO WA VIWANGO.

Karatasi hii imedhamiria kutathmini uwezo wa mtihani wa kuwasiliana na msomaji na kuwasilisha ujumbe

kimaandishi, akizingatia mada aliyopewa.  Mawasiliano haya yatategemea ukwasi wa lugha ya mtahiniwa.

Kwa kutegemea maagizo ya swali lenyewe na umahiri wa lugha, ni lazima kutilia mkazo mtindo, mada na

uwezo na mtahiniwa kufuata maagizo vilivyo. 

Mtahini lazima asome insha yote ili aweze kukadiria viwango mbalimbali vilivyopendekezwa, yaani A, B, C ama D kutegemea mahali popote pale pafaapo kuikadiria insha ya mtahiniwa.

VIWANGO MBALI MBALI

            KIWANGO CHA D – MAKI 01 – 05.

1.         Insha ya aina hii haieleweki kwa vyovyote, ama uwezo wa mtahiniwa wa kutumia lugha ni hafifu sana hivi kwamba mtahini lazima afikirie kile anachojaribu kuandika.

2.         Mtahiniwa hana uwezo wa kutumia maneno ya Kiswahili kwa njia inayofaa.

3.         Lugha imevurugika, uakifishaji usiofaa na insha ina makosa ya kila aina ya  kisarufi, kimaendelezo,

            kimtindo n.k.

4.         Kujitungia swali na kulijibu.

5.         Insha ya urefu wa robo ikadiriwe hapa.

            NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA D

            D – (Kiwango cha chini) Maki 01 – 02.

1.         Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile.

2.         Kujitungia swali tofauti na kulijibu.

3.         Kuandika kwa lugha isiyo Kiswahili au kuchanganya ndimi.

4.         Kunakili swali au maswali na kuyakariri.

5.         Kunakili swali au kichwa tu.

            D (Wastabu)

            Maki 3

1.         Mtiririko wa mawazo haupo.

2.         Mtahiniwa amepotoka kimaudhui.

3.         Matumizi ya lugha ni hafifu mno.

4.         Kuna makosa mengi ya kila aina.

            D+ (D YA JUU) MAKI 04 – 05

1.         Insha huwa na makosa mengi ya kila aina, lakini unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kuwasilisha.

2.         Hoja hazikuelezwa kikamilifu / mada haikukuzwa vilivyo.

3.         Mtahiniwa hana uhakika wa matumizi ya lugha.

4.         Mtahiniwa hujirudiarudia.

5.         Insha itakayozingatia sura lakini ikose maudhui ikadiriwe hapa.

            KIWANGO CHA C KWA JUMLA MAKI 06 – 10.

1.         Mtahiniwa anajaribu kushughulikia mada japo hakuikuza na kuiendeleza vilivyo.

2.         Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia isiyovutia / hana ubunifu wa kutosha.

3.         Mtahiniwa anaakifisha sentensi vibaya.

4.         Mtiririko wa mawazo unaanza kujitokeza japo kwa njia hafifu.

5.         Insha ina makosa mengi ya sarufi, ya msamiati na ya tahajia (hijai)

6.         Insha yenye urefu wa nusu ikadiriwe hapa.

            NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA C

C – (C YA CHINI) MAKI 06 – 07

1.         Mtahiniwa ana shinda ya kuwasilisha na kutiririsha mawazo yake.

2.         Mtahiniwa hana msamiati wa kutosha wala miundo ya sentensi ifaayo.

3.         Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ya msamiati na insha haieleweki kwa urahisi.

            C WASTANI MAKI 08

1.         Mtahiniwa anawasilisha ujumbe lakini kwa nja hafifu.

2.         Dhana tofauti tofauti hazijitokezi wazi.

3.         Mtahiniwa hana ubunifu wa kutosha.

4.         Mtiririko wa mawazo ni hafifu na hana ufundi wa lugha unaofaa.

5.         Amejaribu kuishughulikia mada aliyopewa.

6.         Ana shinda ya uakifishaji.

7.         Anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ya msamiati lakini bado insha inaeleweka.

            C+ (C YA JUU) MAKI 09 – 10        

1.         Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri akizingatia mada lakini kwa njia isiyokuwa na mvuto.

2.         Dhana tofauti tofauti zimejitokeza japo kwa njia hafifu.

3.         Kuna mtiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lugha unaofaa.

4.         Misemo na methali zimetumika kwa njia hafifu.

5.         Ana shinda ya uakifishaji.

6.         Kuna makosa ya sarufi ya msamiati na ya hijai yanayoathiri mtiririko wa mawazo.

            KIWANGO CHA B KWA JUMLA MAKI 11 – 15.

1.         Katika kiwango hiki, mtahiniwa anaonyesha hali ya kuimudu lugha.

2.         Mtahiniwa anatumia miundo tofautitofauti ya sentensi vizuri.

3.         Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha.

4.         Mada imekuzwa na kuendelezwa kikamilifu. Hoja zisipungue nne katika kiwango hiki.

5.         Insha ya urefu wa robo tatu ikadiriwe katika kiwango hiki.

            NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA D.

            B – (B YA CHINI) MAKI 11 – 12

1.         Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri kwa kueleza hoja tofautitofauti akizingatia mada.

2.         Mtahiniwa ana mtiririko mzuri wa mawazo.

3.         Mtahiniwa anatumia mifano michache ya msamiati unaovutia.

4.         Makosa yanadhihirika /  kiasi.

            B WASTANI MAKI 13

            Mtahiniwa anadhihirisha hali ya kuimudu lugha.

2.         Mawazo yake yanadhihirike akizingatia mada.

3.         Mtahiniwa anateua na kutumia mifano michache ya msamiati mwafaka.

4.         Sarufi yake ni nzuri.

5.         Makosa ni machache / kuna makosa machache.

            B+ (B YA JUU) MAKI 14 – 15

1.         Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika waziwazi.

2.         Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia inayovutia na kwa urahisi akizingatia mada.

3.         Mtahiniwa ana mchanganyiko mzuri wa msamiati unaovutia.

4.         Sarufi yake ni nzuri.

5.         Uakifishaji wake wa sentensi ni mzuri.

6.         Makosa ni machache ya hapa na pale.

            KIWANGO CHA a KWA JUMLA MAKI 16 – 20.

1.         Mtahiniwa ana ubunifu wa mawazo yanayodhihirika na kutiririka akizingatia mada.

2.         Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato.

3.         Ana uwezo wa kutumia tamathali za usemi ili kutoa hisia zake kwa urahsi.

4.         Umbuji wake unadhihirisha ukomavu na ukakamavu wake  kimawazo

5.         Insha ina urefu kamili.

            NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA A

            A – (A YA CHINI) MAKI 16 – 17)

1.         Mtahiniwa anadhihirisha ukomavu wa lugha.

2.         Mawazo yake yanadhihirika na anaishughulikia mada kikamilifu.  Hoja tano kuenda juu.

3.         Ana mtiririko mzuri wa mawazo.

4.         Msamiati wake ni mzuri na unavutia.

5.         Sarufi yake ni nzuri.

6.         Anatumia miundo tofautitofauti ya sentensi kiufundi.

7.         Makosa ni nadra kupatikana.

            A WASTANI MAKI – 18

1.         Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri kulingana na mada.

2.         Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato.

3.         Anatoa hoja zilizokomaa.

4.         Anatumia msamiati wa hali ya juu na unaovutia zaidi.

5.         Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi.

6.         Makosa ni nadra kupatikana.

            A+ (A YA JUU) 19 – 20

            Mawazo yanadhihirika zaidi na mada imeshughuliwa vilivyo.

2.         Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato.

3.         Hoja zake zimekomaa na zinashawishi.

4.         Msamiati wake ni wa hali juu na unavutia zaidi.

5.         Sarufi yake ni nzuri zaidi.

6.         Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi, kiufundi.

7.         Makosa yote kwa jumla hayazidi matano.

            VIWANGO MBALIMBALI KWA MUHTASARI.

                        KIWANGO   NGAZI           MAKI

                        A                     A+                   19 – 20                        

                                                A                     18                                                       

                                                A-                    16 – 17                                                

                        B                      B+                   14 – 15                        

                                                B                      13                                                       

                                                B-                    11 – 12                                                

                        C                     C+                   09 – 10

                                                C                     08

                                                C-                    06 – 07

                        D                     D+                   04 – 05

                                                D                     03

                                                D-                    01-02

            USAHIHISHAJI NA UTUZAJI KWA JUMLA.

Mtahini ni sharti aisome insha yote akizingatia vipengee muhimu.  Vipengee hivi ni maudhui, msamiati, mtindo, sarufi na hijai.

            MAUDHUI.

1.         Maudhui ni hoja au mambo yanayozungumziwa, kuelezewa au kuhadithiwa kwa mujibu wa mada iliyoteuliwa.

2.         Maudhui ndio hasa uti wa mgongo wa insha yoyote ile.

3.         Ubunifu wa mtahiniwa hukisiwa kwa kutathmini uzito wa maudhui yake kulingana na mada teule.

            MSAMIATI.

–           Msamiati ni jumla ya maneno yatumiwayo katika lugha husika.

–           Mtahiniwa anatarajiwa kutumia msamiati unaooana na mada teule.

–           Kutegemea ukwasi wa lugha alionao, mtahiniwa anatarajiwa kuikuza mada kwa kuifinyanga lugha kiufundi.

–           Ni muhimu kuelewa kwamba kutokana na maendeleo na ukuaji wa teknolojia na mawasiliano maneno mapya yanaibuka kila uchao.

            MTINDO.

            Mtindo unahusu mambo yafuatayo:

•          Mpangilio wa kazi kiaya.

•          Mtiririko na mshikamano wa mawazo kiaya na katika insha nzima.

•          Hati nzuri na inayosomeka kwa urahisi.

•          Matumizi ya tamathali za usemi, kwa mfano, methali, misemo, jazanda na kadhalika.

•          Kuandika herufi vizuri kwa mfano Jj, Pp, Uu, Ww na kadhalika.

•          Sura ya insha.

•          Unadhifu wa kazi ya mtahiniwa.

SARUFI.

Sarufi ndio msingi wa lugha.  Ufanisi wa mawasiliano hutegemea uwezo wa mtahiniwa wa kutunga sentensi sahihi zenye uwiano wa kisarufi.  Mtahini ataonyesha makosa yote ya sarufi yaliyo katika insha anayosahihisha.  Makosa ya sarufi huweza kutokea katika:

          (i)  Matumizi ya alama za uakifishaji.

          (ii) Kutumia herufi kubwa au ndogo mahali pasipofaa.

         (iii) Matumizi yasiyofaa ya ngeli na viambishi, viunganishi, nyakati, hali, vihusiano na kadhalika.

         (iv) Mpangilio wa maneno katika sentensi.

         (v)  Mnyambuliko wa vitenzi na majina.

        (vi) Kuacha neno linalohitajika au kuongeza neno lisilohitajika katika sentensi.

       (vii) Matumizi ya herufi kubwa:

         (a) Mwanzo wa sentensi.

         (b) Majina ya pekee.

      (i) Majina ya mahali, maji, nchi, mataifa na kadhalika.

      (ii) Siku za juma, miezi n.k.

      (iii) Mashirika, masomo, vitabu n.k.

     (iv)  Makabila, lugha n.k.

      (v) Jina la Mungu.

     (vi) Majina ya kutambulisha hasa wanyama wa kufugwa, kwa mfano yale ya mbwa – Foksi,

           Jak, Popi, Simba, Tomi na mangineyo.

   (vii) Majina halisi ya watu k.m Maria, Rutto.

MAKOSA YA HIJAI / TAHAJIA.

Haya ni makosa ya maendelezo.  Mtahini anashauriwa asahihishe huku akiyaonyesha yanapotokea             kwa mara ya kwanza tu.  Makosa ya tahajia huweza kutokea katika;

(a) Kutenganisha neno kwa mfano ‘aliye kuwa’.

(b) Kuunganisha maneno kwa mfano ‘kwasababu’.

(c) Kukata silabi visivyo afikapo pambizoni kama vile ‘ngan-o’ badala ya nga-no.

 (d) Kuandika herufi isiyofaa kwa mfano ‘ongesa’ badala ya ‘ongeza’.

(e) Kuacha herufi katika neno kwa mfano ‘aliekuja’ badala ya ‘aliyekuja’.

  (f) Kuongeza herufi isiyohitajika kama vile ‘piya’ badala ya ‘pia’.

(g) Kuacha alama inayotarajiwa katika herufi kama vile j, i.

(h) Kukosa kuandika kistari cha kuendelezea neno afikiapo pambizoni au kukiandika mahali             pasipofaa.

(i) Kuacha ritifaa au kuiandika mahali pasipofaa, kwa mfano ngombe, ngom’be, ng’ombe, ngo’mbe n.k

(k) Kuandika tarakimu kwa mfano 27 – 08 – 2013.

ALAMA ZA KUSAHIHISHA.

            =====   Hupigwa chini ya sehemu ambapo kosa la sarufi limetokea kwa mara ya kwanza tu.

            __________   Hupigwa chini ya sehemu au neno ambapo kosa la hijai limetokeza kwa mara ya kwanza tu.

                Hutumiwa kuonyesha hoja inapokamilikia pambizoni kushoto.

                         Hutumiwa kuonyesha kuachwa kwa neno / maneno.

                   Hutumiwa kuonyesha msamiati bora.  Alama hii hutiwa juu ya neno lenyewe.

                  X     Hutumiwa kuonyesha msamiati usiofa. Alama hutiwa juu ya neno lenyewe.

            Maelezo mafupi yanahitajika kuhusu tuzo lililotolewa.  Kila ukurasa uwe na alama ya chini   katikati ili kuthibitisha kuwa mtahini ameupitia ukurasa huo. 

            Maelezo yaonyeshe: Urefu wa insha k.v robo, nusu, robo tatu au kamili na udhaifu wa mwanafunzi.

            UKADIRIAJI WA UREFU WA INSHA.

            Maneno 9 katika kila msitari.                     Ukurasa mmoja na nusu

            Maneno 8 kaitka kila msitari.                     Ukurasa mmoja na robo tatu.

            Maneno 7 katika kila msitari.                     Kurasa mbili.

            Maneno 6 katika kila msitari.                     Kurasa mbili na robo.

            Maneno 5 katika kila msitari.                     Kurasa mbili na robo tatu.

            Maneno 4 katika kila msitari.                     Kurasa tatu na robo tatu.

            Manneo 3 katika kila msitari.                     Kurasa nne na nusu.

            JUMLA YA MANENO.

            Kufikia maneno        174                              Insha robo.

            Maneno                      175 – 274                    Insha nusu.

            Maneno                      275 – 374                   Insha robo tatu.

            Maneno                      375 na kuendelea     Insha kamili.

Scroll to Top