KCSE Prediction Kiswahili pp2 Marking schemes

info

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

KARATASI YA 2

1. UFAHAMU: ALAMA 15

(A).  (i) Wazazi kukwepa jukumu la ulezi.

        (ii) Kutokuwa na sheria/sera iliyo wazi kuhusu usalama wa watoto  

                                                                                                            Hoja yoyote 1×1=1

(B)  (i) Hukosa mapenzi.

       (ii) Hukosa malezi,maelekezo na mwongozo mwafaka maishani

(i)        Huiga tabia bofu K.M kuvuta gundi na kuiba.

(ii)       Njaa

                                                                                                                          Zozote 3×1=3

(C). (i).Kutiliwa maanani kwa  mpango wa vijana wa kujiunga na huduma ya taifa

       (ii).Kuongeza makao ya watoto na kuwapa mafunzo ya kiufundi

       (iii). kuwasajili watoto ili waweze kuunganishwa na familia zao

       (iv).Wafadhili wawape chakula badala ya pesa  taslimu

       (v).Wanaowauzia gundi wahamasishwe dhidi ya matumizi yake

                                                                                                                          Zozote 3×1=3                                                                                                               

(D) (i).Tegemeo lao ni makombo na takataka iliyo mapipani                           (alama 2)

       (ii).Kutolitatua tatizo la watoto wanaorandaranda mitaani kutatuletea  matatizo

         (iii). Mhitaji hachagui chochote                                                                        (alama 2)

(E)     (i). Aidha-pia

         (ii). Gundi- Kitu kiolevu na kinachonata kunachonuswa na watoto kama kileo                                                                                                                                                         1×2=2 

                     2.            UFUPISHO:                          (ALAMA 15)

Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali yafuatayo

Lugha ndio msingi wa maandishi yote. Bila lugha hakuna maandishi. Kila jambo tufanyalo kuhusiana na lugha husitawisha ufahamu wetu wa mambo tusomayo. Mazoezi katika kuandika husitawisha ufahamu katika kusoma kwa sababu katika kuandika ni lazima kuyatumia maneno vizuri na kufahamu ugumu wa usemi. Twajifunza matumizi ya lugha katika kuzungumza na kuwasikiliza wengine wakizungumza. Lugha tusomayo ni anina ya lugha ya masungumzo.

Kuna ujuzi mwingi katika kuzungumza kama vila michezo ya kuigiza, hotuba, majadiliano na mazungumzo katika darasa. Haya yote husaidia katika uhodari wa matumizi ya lugha. Ujuzi wa kila siku utasaidia katika maendeleo ya kusoma na usitawi wa msamiati. Ikiwa mwanafunzi amemwona ndovu hasa, atakuwa amejua maana ya neno ndovu vizuri zaidi kuliko mwanafunzi ambaye hajawahi kumwona ndovu bali ameelezwa tu vile ilivyo. Vilevile ujuzi wa kujionea sinema au michoro husaidia sana katika yaliyoandikwa. Ikiwa mwanafunzi ana huzuni au ana furaha, akiwa mgonjwa au amechoka au amefiwa, haya yote ni ujuzi. Wakati juao mwanafunzi asomapo juu ya mtu ambae amepatikana na mambo kama huyo hana budi kufahamu zaidi.

Karibu elimu yote ulimwenguni huwa imeandikwa vitabuni. Hata hivyo, lugha zote hazina usitawi sawa kuhusu fasihi. Kwa bahati mbaya lugha nyingine hazijastawi sana na hazina vitabu vingi. Fauka ya hayo , karibu mambo yote yanayohusiana na elimu huweza kupatikana katika vitabu kwenye lugha nyingine.

Inambidi mwanafunzi asome vitabu au majarida juu ya sayansi au siasa au historia, lakini haimbidi kusoma tu juu ya taaluma fulani anayojifunza . Inafaa asome juu ya michezo, mambo ya mashairi na juu ya mahali mbalimbali ili kupata ujuzi wa mambo mengi.

a)         Fupisha aya za kwanza mbili kwa kutumia maneno 65 (alama 10, 1 ya utiririko)

            Matayarisho 

         Kila jambo tufanyalo katika lugha hustawisha ufahamu wake.

         Mazoezi ya kuandika hustawisha ufahamu wa kusoma.

         Twajifunza matumizi ya lugha katika kuzungumza na kuwasikiliza wengine.

         Lugha iliyoandikwa ni ya aina ya mazungumzo.

         Ujuzi mwingi katika kuzungumza hupatikana shuleni.

         Ujuzi wa kila siku husaidia katika maendeleo ya kusoma na msamiati.

         Husaidia kufahamu yaliyoandikwa.

         Hali ya mwanafunzi kujionea sinema ni ujuzi.

         Matatizo na shida ambazo wanafunzi hupitia pia ni ujuzi.

b)         Kwa kuzingatia habari zote muhimu na bila kupoteza maana asilia, fupisha aya ya mwisho

            (Maneno 30) (alama 5 utiririko)

            Matayarisho

         Karibu elimu yote imeandikwa vitabuni.

         Lugha zote hazina ustawi mwingi.

         Nyingine hazina vitabu ama zina vitabu vingi.

         Mwanafunzi anayesoma anafaa kusoma mengi kando na taaluma anayoisoma.

3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

(a)        Toa mifano miwili miwili ya                                                                                    (al.2)

i.          Sauti ghuna ambazo ni vipasuo  /b/ /d/ /g/

ii.         Sauti sighuna ambazo ni vikwamizo /f/ /th/ /sh/ /h/

(b)       Onyesha mofimu katika neno  Aliyemcha 

a-nafsi/ngeli  li-wakati ye-kirejeshi  m-yambwa mtendewa ch-mzizi a-kiishio

(c)        Andika sentensi yenye muundo ufuatao                                                            (al.2)

KN(W+V) + KT (t +RH)

Yule mtukutu alikuwa chini ya mti

(d)       Tumia neno shirika kama nomino na kama kielezi katika kutunga sentensi moja                                                                                                                                                      (al.2)

Wafanyakazi wa shirika lile walifanya kazi kwa ushirikiano/kishirika

(e)        Kwa kutunga sentensi vumisha nomino ng’ombe kwa kivumishi cha idadi bainifu.                                                                                                                                   (al.1)

Ng’ombe sita wamepelekwa malishoni

(f)        Andika sentensi ifuatayo katika hali ya kutendewa                                            (al.1)

Mtoto wa waziri amekufa

Waziri amefiwa na mtoto wake

(g)       Yakinisha sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu wingi                    (al.2)

Msomi hakutukuzwa siku hiyo

Wasomi watakuwa wametuzwa siku hiyo

(h)       Tunga sentensi moja inayobainisha maana mbili tofauti za neno chuma         (al.2)

Kifaa cha madini

Tafuta pesa

Toa matunda mtini

Bakari alichuma matunda ya parachichi kwa kutumia kifaa kilichotengenezwa kwa chuma

(i)        Tambua kiima na aina za yambwa katika sentensi ifuatayo.                             (al.4)

Mwalimu mkuu hupigiwa nguo pasi na Maria

Mwalimu mkuu – yambwa tendewa/kitondo

nguo –yambwa tendwa/kipozi

pasi – yambwa ala/ kitumizi

Maria – kiima

(j)         Kwa kutumia mifano mwafaka fafanua miundo yoyote miwili ya kirai nomino                                                                                                                                                 (al.2)

Nomino pekee (N)

Kiwakilishi (W)

N+U+N – Nomino +Kiunganishi +Nomino

N+V – Nomino + Kivumishi

N+V+V – Nomino + Kivumishi + Kivumishi

N+V+E – Nomino + Kivumishi + Kielezi

N+S – Nomino + Kishazi

(k)       Andika sentensi ifuatayo kwa wingi                                                                     (al.2)

Mgeni huyo na mwingine walikula wali kwa uma

Wageni hao na wengine walikula wali kwa nyuma

(l)        Andika neno lenye silabi funge yenye muundo wa konsonanti moja              (al.1)

m-toto

m-tu

(m)      Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika udogo wingi                                           (al.2)

Ng’ombe wangu ana ndama mdogo

Vigombe vyangu vina vidama vidogo

(n)       Tunga sentensi zenye mipangilio ifuatayo;                                                           (al.4)

i.          Kishazi tegemezi na kishazi huru

Mtoto aliyewasili leo                              amerudi kwao

K.T                                                                  K.H

ii.         Kishazi tegemezi na kishazi tegemezi

Angalilima kwa bidii                                      angalivuna mavuno tele

K.T                                                                               K.T

(o)       Eleza matumizi ya ‘ki’ katika sentensi ifuatayo:                                                  (al.3)

Nyamunga na kitoto wamekuwa wakila, wakiimba kikasuku

kitoto – udogo

wakila , wakiimba – vitendo viwili kufanyika kwa wakati mmoja

kikasuku – ki ya kielezi

(p)       Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia mchoro wa matawi.                      (al.4)

Mtoto wa mjomba alikuja kwetu nyumbani jana

                                                                S

            KN                                                                         KT

N                         V                                      N                  T                         V                  E            E                                                                                                                              Mtoto                   wa                                    mjomba      alikuja                 kwetu    nyumbani   jana       

(q)       Andika kwa msemo wa taarifa.                                                                              (al.2)

‘Yafaa tumwendee mama mkubwa ili atushauri juu ya jambo hili,’ Amina alipendekeza.

Amina alipendekeza kuwa ilifaa wamwendee mama mkubwa ili awashauri juu ya jambo hilo

(r)        Andika kinyume cha:                                                                                              (al.1)

Chakula hiki kitamu nitakimeza

Chakula hiki kichungu nitakitema

(s)        Tunga sentensi ukitumia viwakilishi vifuatavyo.

(i)        Kiwakilishi nafsi huru

Mimi hupika vizuri/sisi/wewe/nyinyi/yeye/wao

(ii)       Kiwakilishi nafsi kiambata

Aliondoka jana/wa/ni/tu/u/m

         4.    ISIMUJAMII

(a)– kuhamisha msimbo ni kutumia lugha fulani katika mazungumzo kisha ukaanza kutumia lugha nyingine tofauti na ile ya kwanza.

   -Kuchanganya ndimi ni matumizi ya maneno au msamiati wa lugha zaidi ya moja katika mazungumzo.                                                                                              2 x 1= 2

(b)       (i) Ukosefu wa msamiati unaofaa katika lugha hiyo.

(ii) Wazungumzaji kutojua lugha husika vizuri.                                                2 z 1 = 2

(c)        (i) Wakati – kwa mfano kuna maamkizi ya asubuhi kama vile “subalkheri”, na ya jioni kama vile “masalkheri”.

(ii) Umri – kwa mfano mtu wa umri mdogo humwamkua mkubwa wake “shikamoo” naye hujibu, “ marahaba”.

                                                                                                                                    2 x 1 =2)

(d)       (i) Mtu mmoja hutawala mazugumzo kama vile hakimu, wakili, kasisi, shehe n.k.

(ii)Mazungumzo hurejelea kanuni  zilizoandikwa kama vile sheria za nchi, Korani, Biblia n.k.

(iii) Lugha ya heshima hutumika kama vile mheshimiwa, dada, ndugu n.k.

(iv)Mazungumzo hutolewa mahali maalum kama vile mahakamani, msikitini, kanisani au  hekaluni.

(v)Lugha sanifu hutumika ili ieleweke vizuri.

(vi)Mazungumzo huweza kueleweka tu na wahusika wenyewe.

                                                                                                                        (zozote 4 x 1= 4)

–           Ondoa nusu alama kwa kila kosa tofauti la hijai hadi makosa 4, yaani alama 2

–           Ondoa nusu alama kwa kila kosa tofauti la sarufi hadi makosa 4, yaani alama 2.