KCSE Prediction Kiswahili pp1 Questions

info

                                                      Maagizo

            (a)        Andika Insha mbili.  Insha ya kwanza ni ya  lazima.

            (b)        Kisha chagua Insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.

            (c)        Kila Insha isipungue maneno 400.

            (d)        Kila Insha ina alama 20.

            (e)        Kila Insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

            (f)         Karatasi hii ina kurasa 2 zilizopigwa chapa.

1.         LAZIMA

Mwandikie barua mhariri wa Gazeti la Baraka ukimweleza sababu za watoto wengi katika kaunti yako kuacha shule na kujiingiza katika ajira za mapema.

2.         Vipakatalishi vimeleta manufaa mengi nchini .

            Fafanua.

3.         Andika insha itakayothibitisha ukweli wa methali:\               

            Mcheka kilema hafi bila kumpata.

4.         Andika kisa kitakachoanzia kwa maneno yafuatayo:

            Kushoto kulikuwa na jitu la miraba minne ambalo lilitema cheche za matusi ungedhania ni

            karakana …