Please Limited time Offer!

Semi – Fasihi Simulizi

Sifa

 1. Huwa fupi kwa kuwasilisha ujumbe mrefu kwa maneno machache
 2. Ni tanzu tegemezi kwa hutegemea tanzu nyingine kama vile hadithi, mazungumzo, n.k.
 3. Hazibadiliki vivi hivi
 4. Baadhi ni kielelezo cha maadili k.v. methali
 5. Hutumia lugha ya kimafumbo
 6. Huibua taswira
 7. Huwa na mchezo wa maneno
 8. Baadhi huwa na muundo maalum k.v. methali na vitendawili
 9. Nyingine ikikosa kutumika hutoweka k.v. misimu

Umuhimu

 1. Kuonya k.m methali, ‘Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.’
 2. Kukuza uwezo wa kufikiri k.m. vitendawili na chemsha bongo
 3. Kutafsidi lugha au kupunguza ukali wa maneno k.m. nahau ‘jifungua’ badala ya ‘zaa’
 4. Kuburudisha k.m. vitendawili, chemsha bongo na vitanza ndimi
 5. Kuhifadhi siri k.m. nahau, misemo, misimu
 6. Kuelimisha k.m. kutofanya mambo kwa pupa-mla kwa pupa hadiriki kula tamu
 7. Kuongeza utamu katika lugha
 8. Kuboresha matamshi k.m. vitanza ndimi
 9. Kukuza lugha k.m misimu
 10. Kukuza utangamano katika jamii kwa kuleta watu pamoja wakati zinawasilishwa

Vipera vya Semi

a) Methali

– Semi fupi ambazo hueleza kwa muhtasari au mafumbo ukweli fulani wa kimaisha.

Sifa

 1. Huwa fupi k.m. ‘Msafiri kafiri.’
 2. Hutumia tamathali za usemi.
 3. Hutumkia lugha ya kimafumbo.
 4. Huwa na maana ya ndani na nje.
 5. Kunazo hufanana kimaana k.m. ‘Haraka haraka haina baraka’ na ‘Polepole ndio mwendo.’
 6. Hupingana zenyewe k.m ‘Polepole ndio mwendo’ na ‘Chelewa chelewa utamkuta mwana si wako.’
 7. Huwa na sifa za kishairi k.v. ukwapi, utao na vina -Haba na haba, hujaza kibaba.
 8. Sifa za utegemezi kwa kuingiliana na tanzu nyingine za fasihi
 9. Huwa na muundo maalum wa sehemu mbili:
  i) Wazo k.m ‘Haba na haba…’
  ii) Kukamilisha wazo ‘…hujaza kibaba.’

Umuhimu

 1. Kukuza uwezo wa kufikiri kwani mpokezi hufikiri ili kupata maana ya ndani
 2. Kuonya dhidi ya matendo yasiyofaa k.m. Mchimba kisima huingia mwenyewe na Ukiambiwa jiambie usijeishia kumbe.
 3. Kufariji walio katika hali ngumu, k.m Baada ya dhiki farajaHakuna marefu yasiyo na nchaLiandikwalo ndilo liwaloAjaliwalo ndilo apatalo
 4. Kuhimiza watu kujitahidi maishani/kuonyesha jambo jema huja kwa kufanyiwa kazi k.m. Mtaka cha mvunguni sharti ainameChumia juani ulie kivulini
 5. Kupamba lugha iwe na mvuto kwani huwa na usanii mkubwa
 6. Kuhimiza ushirikiano k.m. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifuJifya moja haliijiki chungu
 7. Kuelimisha mtu ajue jambo muhimu k.m. Usione kwenda mbele kurudi nyuma si kaziPema usijapo pema ukipema si pema tena
 8. Kushauri k.m. Enga kabla ya kujenga na Mchama ago hanyeli
 9. Kufupisha maadili katika ngano
 10. Kubuni lakabu k.m. kikulacho
 11. Kufunza maadili k.m. kuwa na subira – Subira huvuta heri.
 12. Kuhimiza kutokata tama k.m. Bandu bandu huisha gogoPapo kwa papo kamba hukata njiwe
 13. Kuonyesha umuhimu wa kuthamini jamaa zako kuliko marafiki k.m. Damu ni nzito kuliko majiMla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe
 14. Kuonyesha umuhimu wa kuthamini vitu vyako – Usiache mbachao kwa msala upitao na Afadhali dooteni kama ambari kutanda
 15. Kukashifu ubinafsi k.m. Mwamba ngoma huvutia kwakeKila mchukuzi husifu mzigo wake
 16. Kukashifu kiburi k.m. Maskini akipata matako hulia mbwataZingwi zingwi lipe nguo utaona mashauo

Mbinu za Lugha/Fani /Tamathali za Usemi katika Fasihi

– Maneno au vifungu vya maneno vinavyotumiwa kutia fasihi urembo ili kufanya ujumbe ueleweke vyema zaidi.

 • Tashbihi – Ulinganishi kwa kutumia viunganishi kama, mithili, mfano na sawa k.m Kawaida ni kama sheria
 • Sitiari/ Istiara – Ulinganishi usio wa moja kwa moja k.m Mgeni ni kuku mweupe
 • Tashhisi/Uhaishaji – Kukipa kitu sifa ya uhai k.m Siri ya mtungi muulize kata
 • Taashira/ Ishara – Kitu kuwakilisha kingine k.m Kimya kingi kina mshindo mkubwa
 • Chuku/udamisi – Kutia chumvi au kufanya kitu kionekane kikubwa sana au kidogo sana k.m Usipoziba ufa utajenga ukuta
 • Takriri – Urudiaji wa neno au mafungu ya maneno k.m Haba na haba hujaza kibaba
 • Tanakuzi – Maneno yaliyo kinyume k.m Mpanda ngazi hushuka
 • Tabaini – Msisitizo kwa njia ya kinyume kwa kutumia kikanushio ‘si’
 • Ritifaa – Kusemesha asiyekuwapo kama yupo
 • Taharuki – Kuacha msomaji akiwa na hamu ya kutaka kujua kipi kitakachojiri halafu
 • Mbinu rejeshi – Kukumbusha mambo yaliyopita k.m
 • Balagha – Maswali yasiyohitaji majibu k.m Pilipili usiyoila yakuwashiani?
 • Taswira – Ujenzi wa picha akilini k.m Mpanda farasi wawili hupasuka msamba
 • Kinaya – Mhusika kutumia maneno au matendo yaliyo kinyume cha inavyotarajiwa k.m Asante ya punda ni mateke
 • Kejeli – Kudharau au kubeza k.m Ucha Mungu si kilemba cheupe
 • Jazanda – Kufananisha vitu kwa mafumbo k.m. katika biblia k.m Kupanda mchongoma kushuka ndio ngoma
 • Kweli kinzani – Hoja mbili zinazopingana/kutowezekana k.m Wagombanao ndio wapatanao

Vigezo vya Kuainishia Methali / Kuziweka Pamoja na kuzichambua

 1. Mandhari/mazingira k.m. kilimo. k.m Ukipanda pantosha utavuna pankwisha
 2. Maudhui k.m. ulezi k.m Samaki mkunje angali mbichi
 3. Fani/tamathali k.m Haba na haba hujaza kibaba
 4. Jukumu k.m. kuonye k.m Asiyesikia la mkuu huvunjika guu
 5. Maana k.m. sawa k.m Haraka haraka haina baraka

ii) Vitendawili

 Semi ambazo hutolewa kwa mtu kwa mfano wa swali ili azifumbue.

Sifa

 • Huwa vifupi kimaelezo.
 • Hutumia lugha ya kimafumbo.
 • Hutolewa mbele ya hadhira.
 • Hutumia ufananisho wa kijazanda.
 • Kunazo huhusiana na methali k.m. mzee amekufa vyombo vimevunjikavunjika.
 • Huwa na wakati maalum wa kutolewa yaani jioni.
 • Huwa na mchezo wa maneno k.m. Ukiona njigi utadhani njege
 • Hujisimamia vyenyewe
 • Kunavyo huwa na jibu zaidi ya moja
 • Hutumia tamathali za lugha kwa ufanifu mkubwa
 • Huweza kuwa na fomyula/muundo maalum
  • k.m. Mteguaji: Kitendawili
   Mteguaji: Tega

Umuhimu

 1. Kuburudisha jioni baada ya kazi
 2. Kukuza ubunifu wa kuvitunga kwa kulinganisha vitu katika mazingira ili kuviunda
 3. Kuimarisha uwezo wa kukumbuka
 4. Kukuza uwezo wa kufikiri kwani mfumbiwa huhitaji kufikiri sana ili kupata jibu
 5. Kuleta umoja na ushirikiano katika jamii kwa kuleta watu pamoja wakati vinategwa
 6. Kuimarisha ujuzi wa kujieleza kwa lugha
 7. Kupanua ujuzi wa mazingira wa mtoto
 8. Kuendeleza utamaduni wa jamii k.m. Nyumbani mwetu mna papai lililoiva lakini. siwezi kulichuma
 9. Kukejeli au kudharau tabia mbaya k.m. Wazungu wawili wanachungulia dirishani
Scroll to Top