This is a compilation of Questions from past KCSE, Mocks, Pre/Post-mocks and Internal Exams.
MASWALI YA TAMTHILIA YA BEMBEA YA MAISHA NA TIMOTHY AREGE
- “…haikuwa mara moja mnavyofikiria. Ilianza pale chuoni. Wenzangu walinipa mvinyo kunirai kuonja ulevi.”
- Eleza maudhui manne yanayojidokeza katika dondoo hili. (alama 4)
- Eleza athari za mhusika anayerejelewa kujitosa katika suala linalooredheshwa kwenye dondoo. (alama 6)
- Kwa kurejelewa mifano tano katika tamthilia ya Bembea ya maisha, eleza tofauti iliopo katika maisha ya ndoa ya zamani na sasa (alama 10)
- Jadili sababu kumi zilizompeleka mwandishi T. Arege kuandika Tamthilia hii. (alama 20)
- “Ana nini naye amebariki wana Watoto wenye akili nzuri? Wote wamehitimu vizuri na kuleta faraja.”
a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake. ( alama 4)
b) Fafanua sifa tatu za mzungumzaji maneno haya. (alama 6)
c) Jadili jinsi msemewa maneno haya anavyoendeleza ploti yatamthilia ya Bembea ya Maisha. (alama 10)
- “Zamani walikuwa maskini kweli. Leo hii wanaafadhalikiasikwambahuwezikujuakuwajanahawakuwawatuwakutajwa au kupigiwamfano…”
a) Taja mnenajinamnenewamanenohaya (Alama 2)
b) Eleza umuhimuwawanaorejelewakatikadondoohilikatikakuijengatamthiliayaBembeayamaisha (alama10)
c) Kwa kutoamifanominne, jadilisuala la utamadunikamalinavyodhihirikakatikatamthiliayaBembeaya Maisha. (alama 8)
- ‘’Dunia ikijua anakusaidia jikoni itasema unashusha hadhi yake na kwa mizani ya jamii utakuwa unajivulia nguo. ‘’
a. Eleza muktadha wa maneno haya. Alama 4
b. Tambua tamathali mbili za usemi katika dondoo. Alama 2
c. Fafanua sifa zozote nne za msemaji wa maneno haya. Alama 4
d. Tathmini umuhimu wa mandhari kwa kurejelea nyumbani kwa Sara. Alama 10
- ‘’ Kila mbegu ipandwayo haina budi kuzaa na izaapo mazao yake huvunwa. Mtu huitakasa sahani akijua itamfaa tena.’’
a. Eleza muktadha wa maneno haya. Alama 4
b. Fafanua umuhimu wa msemaji katika kujenga ploti. Alama 4
c. Tambua mbinu moja ya kimtindo katika dondoo. Alama 2
d. Kwa kutoa mifano kumi eleza namna mbinu iliyotambuliwa katika sehemu (c) imetumiwa kuendeleza tamthilia hii. Alama 10
BEMBEA YA MAISHA KCSE Questions and Answers
- Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo:
“Unayafanya makubwa bure mwenzangu. Unafahamu vizuri kuwa hiyo si hulka yangu. Sasa
mimi nina haja gani kuuvunja mji?”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama4)
(b) Bainisha toni ya msemaji. (alama2)
(c) Msemaji amepitia dhiki mbalimbali katika jamii yake, Tambua dhiki alizopitia.
( (alama4)
(d) Onyesha namna maudhui ya mgogoro yanavyojitokeza katika tamthilia nzima(ala10)
- “Sasa kichwa hicho kisizunguke? Kikae pale pale ndiyo ujue ni kichwa? Kichwa kazi yake
kuzunguka. Lipi lisilozungusha kichwa? Kutafuta lisilokizungusha kichwa ni kama kuwinda hewa
kutaka kufumbata kwenye konzi.”
(a) Changanua mtindo katika dondoo hili. (alama 3)
(b) Eleza umuhimu wa msemaji wa maneno haya katika kukuza tamthilia ya Bembea ya Maisha..
(alama 5)
(c) Asasi ya ndoa inakumbwa na changamoto nyingi katika maisha. Thibitisha kwa kurejelea
tamthilia ya Bembea ya Maisha. (alama 12)
- ‘’ Lakini ndiyo tabia yenu wanawake.Miaka inaposonga kama hivi mnatuona kama…kama…kama vile tambara bovu.’’
a. i)Yaweke maneno haya katika muktadha wake. (Alama 4 )
ii)Tambua mbinu mbili za kimtindo katika dondoo. (Alama 2)
b) Fafanua umuhimu wa msemaji katika kujenga ploti. (Alama 4)
- Utamanduni huthaminiwa sana na jamii ya tamthilia ya Bembea ya Maisha. Jadili ukweli wa kauli hii kwa kutoa mifano kumi mwafaka tamthiliani. (alama 10)
- Beni:Afadhali hao.Mjukuu wangu hatofautishi kondoo,mbuzi na mbwa.Wote hao kwake yeye ni mbwa!(wanacheka wote)
Yona: Inachekesha.
Swali
Mazungumzo haya kati ya Beni na Yona yanabainisha tofauti iliopo kati ya suala la usasa na ukale. Kwa kutoa mifano kumi inayoonyesha usasa na kumi inayoonyesha ukale,linganua masuala haya. (alama 20)
BEMBEA YA MAISHA KCSE Questions and Answers
- “Maisha ya sasa hayana fundi.Yanamwendesha kila mtu kama tawi lililosukumwa hadi
likang’oka kutoka taagani na kupeperushwa na upepo…Ulimwengu wa sasa haubagui.
Wadogo kwa wakubwa”.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Huku ukitoa mifano, changanua mbinu tano za uandishi ambazo zimejitokeza
katika nukuu. (alama 10)
c) Kukatika kwa bembea haiwi mwisho wa mchezo huunganishwa na mchezo kuendelea.
Kwa kutoa mifano sita onyesha jinsi wahusika mbalimbali walivyounganisha bembea
yao ya maisha. (alama 6)
- Mabadiliko katika maisha ya mwanadamu hayana budi kumfika.Wakati mwingine
mabadiliko haya huleta heri au mahangaiko. Jadili kwa kutoa mifano jinsi wahusika
mbalimbali walivyokumbwa na mabadiliko haya ukirejelea tamthilia ya ‘Bembea ya
Maisha’. (alama 20)
BEMBEA YA MAISHA KCSE Questions and Answers
- Eleza umuhimu wa mhusika Sara katika kujenga vipengele vifuatavyo. (alama 20
(i) Ploti
(ii) Maudhui
- “Maisha ya sasa hayana fundi. Yanamwendesha mtu kama tawi lililosukumwa
hadi likang’oka kutoka Tagani na kupeperushwa na upepo.
(i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(ii) Tambua vipengee vya kimuundo katika dondoo. (alama 2)
(iii) Eleza sifa nne za msemewa. (alama 4)
(iv) Thibitisha kauli ya msemaji ukirejelea tamthilia nzima. (alama 10)