Part 1 ya Mwongozo Wa Bembea ya Maisha-Comprehensive Guide
MTIRIRIKO WA MAONYESHO
SEHEMU I
Onyesho I
Nyumbani kwa Sara, Sara ameketi kwenye kochi baada ya kumeza vidonge vya dawa kwa sababu ya maradhi yanayomsumbua. Yona anayeonekana mchovu na mwenye kukinai anaingia kwa nyumba.
Onyesho linaanza kwa kuonyeshwa namna Yona asivyofurahia hali katika nyumba yake. Analalamikia Sara kuwa hajamwandalia chakula. Yona hababaishwi na hali ya Sara ya ugonjwa, haja yake ni chumba kivuke moshi. Sara anamweleza namna mwili wake ulivyo, hapo mazungumzo kuhusu mwana wao, Neema, yanaanza. Yona anatoa wazo lake kwa Sara amwite bintiye aje ampeleke hospitalini. Sara anakataa wazo hilo kwa kukiri kuwa bintiye ana familia yake ambayo anafaa kuishughulikia.
Maoni ya Sara yanazua mgogoro baina yake na Yona kuhusiana na mtoto wao Neema. Yona anashikilia kuwa ni jukumu la bintiye kuwajibikia matibabu ya mamake, naye Sara anashikilia kuwa bintiye ana majukumu ya kwake na tayari amewafanyia mengi, kwa hivyo, awachwe apumzike.
Mgogoro huu unasawazishwa onyesho linapoelekea kuisha. Sara na Yona wanakubaliana kuwa wanafaa kumpa binti yao baraka zao.
Onyesho linamalizika kwa kuonyeshwa Yona akirejelea suala la chakula. Sara anamweleza asubiri kwa kuwa amempelekea Dina salamu aje awafanyie chochote.
MASUALA MAKUU
Onyesho hili linakunjua jamvi la mjadala kuhusiana na majukumu ya watoto kwa wazazi wao. Inabainika kuwa katika jamii nyingi watoto wa kiume ndio wanaotarajiwa kuwatunza wazazi wanapozeeka.
Inachukuliwa kuwa watoto wa kike walioolewa wanapaswa kupewa fursa ya kushugulikia jamii za kule walikoolewa. Ingawa Neema ni mtoto wa kike, anaonekana kuyamudu majukumu yake kama ambavyo mtoto wa kiume angaliweza kuyamudu. Msemo wa ‘kutoa ni moyo usambe ni utajiri’ unadhihirishwa na matendo ya Neema. Mazungumzo baina ya Sara na
Yona yanadhihirisha kuwa hata ajira za kiwango cha chini kama zile za kufanya kazi shambani na nyumbani pia huwa na changamoto zake. Baadhi ya waajiriwa huwaibia waajiri wao huku wengine wakidhihirisha hali za uvivu na kushindwa kutekeleza wajibu wao kama inavyotarajiwa.
ONYESHO II
- Onyesho hili linatukia nyumbani kwa Dina. Kiwa alikuwa amefika nyumbani kumjulia hali mama yake.
- Onyesho hili linaanza kwa kuonyeshwa namna Kiwa anavyogusagusa chakula na kudai ametosheka. Katika harakati ya mazungumzo juu ya chakula, Dina na Siwa wanajikuta wakizungumza kuhusu familia ya Yona na Sara. Dina anamweleza mwanawe Kiwa namna familia hiyo ilivyodunishwa na wanajamii kwa kukaa muda mrefu bila kujaliwa na watoto na hata baada ya kufanikiwa na watoto wasichana, jamii iliendelea kuwasuta na kuwakejeli kwa kuwa hawakujaliwa na mtoto wa kiume atakayerithi fimbo ya baba yake. Kusemwa huku na wanajamii kunasababisha Yona kuingia katika ulevi, ulevi ambao unamsukuma kumdharau na kumchapa bibi yake kichapo cha mbwa.
- Onyesho linaisha kwa kuonyeshwa Dina akimuaga Kiwa ili aweze kwenda kumsaidia Sara katika harakati ya mapishi kwa kuwa Sara alikuwa anaugua.
MASUALA MAKUU
Onyesho hili linamulika masuala matatu muhimu. Taasubi ya kiume na mila potovu, ukosefu wa ufahamu kuhusu chanzo cha jinsia ya watoto na umuhimu wa bidii maishani. Kulingana na somo la Biolojia, chembechembe za kromosomu zinazofanya uamuzi wa jinsia ya mtoto hutokana na wazazi wa kiume ambao wamebeba kromosomu aina ya Y isababishayo kuzaliwa kwa mtoto wa kiume. Mwanamke hana uamuzi kuhusiana na jambo hili. Hali ya kuwafedhehesha na kuwanyanyasa wanawake kutokana na kuzaliwa kwa watoto wa kiume halina msingi wowote. Tatizo hili linatokana na ubabe dume na taasubi ya kiume. Hali hii inatiliwa mbolea na utamaduni potovu wa jamii kutaka kumrithisha mtoto wa kiume na kumkandamiza mtoto wa kike. Suala la bidii maishani linajitokeza kama kiungo muhimu cha ujenzi wa maisha.
Mtiririko wa Maonyesho Katika Bembea ya Maisha
Dina anajitolea kuwasaidia Sara na Yona katika kazi za nyumbani kutokana na hali mbaya ya afya ya rafikiye Sara. Tendo hili linadhihirisha udugu na ujirani mwema.
ONYESHO III
Onyesho hili linatokea nyumbani kwa Sara, jikoni. Dina yupo katika harakati ya mapishi naye
Sara amejikunyata kwenye kibao. Mchuzi u tayari. Sara anamshukuru Dina kwa kufika kumsaidia. Dina anapokea shukrani na kumpa Sara maneno ya kumtia nguvu. Dina anamweleza Sara kuwa kila kitu hufanyika kwa mpango wa Manani. Anamweleza atazame faraja ilivyovuka kwake kwa vile watoto wake wamefaulu maishani. Anampa matumaini kwamba atapona kwa kuwa hospitali ambayo Neema anampeleka ina watalaamu.
Mazungumzo ya matumaini yanaendelea kunoga huku Dina akiendelea na mapishi. Dina anauliza Sara alikokwenda Yona na hapo mazungumzo kuhusu mwanamume na utamaduni yanazuka.
Tunaelezwa namna utamadumi ulivyowajenga wanaume kama watu wasiofaa kuingia jikoni.
Onyesho hili linatimia Sara akimweleza Dina kuhusu mipango iliyopangwa na Neema kuhusu namna atakavyorudi kliniki kupata matibabu.
MASUALA MAKUU
Katika onyesho hili inadhihirika wazi kwamba taasubi ya kiume imemtawala Yona na kumfanya kutoona hali ya unyonge wa mkewe.
Inamlazimu Sara kuomba usaidizi kwa jirani ndipo waandaliwe chakula ilhali ni kazi ambayo Yona angeifanya bila malalamishi na kuficha siri ya familia yake. Suala la wanaume kutosaidia katika shughuli za nyumbani hutokana na mila na desturi ambazo zinamdhalilisha mwanamke. Mwanamume anapomsaidia mkewe jikoni huona ni kama kwamba hadhi yake imeshushwa.
La kutia moyo ni kwamba, ingawa jamii inamdhalilisha mwanamke, ni dhahiri kuwa mwanamke wa sasa amejizatiti na kujiinua na kufikia kiwango cha kutajika. Neema anakuwa mfano mzuri katika jamii kwa kuyabeba majukumu yake binafsi na yale ya nyumbani alikotoka.
Anahakikisha mama yake anatibiwa na kumfanya Yona amuonee fahari si tu kama msaidizi bali nguzo muhimu ya kutegemewa hata ingawa ni mtoto wa kike, tena aliyeolewa.
Umuhimu wa ujirani mwema pia unazungumziwa. Dina anajitokeza kuwa jirani na rafiki wa kutegemewa wa Sara. Ni wazi kuwa Sara na Yona wanaishi vizuri na majirani wao.
Mtiririko wa Maonyesho Katika Bembea ya Maisha
SEHEMU II
ONYESHO I
Nyumbani kwa Neema, Neema na mamake wameketi ukumbini wanazungumza. Sara amefika mjini kwa ajili ya matibabu na amechoka kutokana na safari ndefu. โฎ Neema anashangazwa na kuchelewa kwa Lemi kutoka shuleni. Anakumbushwa na Bela kuwa Lemi anajiandaa kwa hafla itakayofanyika shuleni na ambayo Neema ameisahau kwa sababu ya
Neema anamsaili mamake kuhusu sababu za vurumai za mara kwa mara za Yona. Sara anamweleza kuwa vurumai hizo zilizomsababishia maradhi ya moyo zilitokana na ulevi; kwamba Yona alitaka amzalie mtoto wa kiume. Jamii nayo ilimsukuma Yona aoe mke mwingine ili azaliwe mtoto wa kiume ambaye Sara hakufanikiwa kupata. Yona aliposhindwa kuhimili shinikizo hizo aliingia katika ulevi hadi akafutwa kazi. Mbali na haya, Sara anamtetea Yona kwa hali na mali kuhusu tabia yake ya ulevi na vurumai.
Ni katika onyesho hili tunapomwona Neema akilalamika kuhusu Bunju, mumewe. Kulingana na Neema, Bunju anaonekana mgumu wa pesa. Anajitetea kwamba amebanwa na mahitaji mengi ambayo hayamwachi na fedha za ziada. โฎ Tathmini
Kupitia kwa mazungumzo haya, masuala kadhaa yanajitokeza yakiwemo maeneo ya mashambani yaliyopuuzwa kimaendeleo, bidii maishani, taasubi ya kiume pamoja na athari za uraibu wa pombe. Usemi ‘mrina haogopi nyuki,'(uk. 18) unaotumiwa na Sara unaelezea bidii inayohitajika ili mtu afaulu maishani. Kwamba, sharti mtu akabiliane na magumu anayokumbana nayo. Sara anayasema haya anapogundua kuwa Lemi ana kazi nyingi za kufanya huko shuleni.
Kwa sababu ya kazi hizo, inakuwa vigumu kwa Sara kuonana na mjukuu wake.
Suala la uwajibikaji miongoni mwa wanasiasa linajitokeza pia. Suala hili linaangaziwa kupitia usafiri unavyotatizwa na miundo misingi duni katika sehemu za vijijini.
Inabainikakwambayonaanajitokomezaulevinikutokananamsukumo wa wanajamii kwa kukosa kuzaa mtoto wa kiume. Huu ni utamaduni uliopitwa na wakati. Pombe inakuwa kimbilio la kumsahaulisha malengo aliyoshindwa kuyafikia. Sara anasisitiza kwamba wazazi wana wajibu wa kumlea mtoto wa jinsia yoyote ile bila ubaguzi.
ONYESHO II
Onyesho hili linafanyika nyumbani kwa Neema akiwa na Bela, mfanyakazi wake. Kupitia mazungumzo yao inabainika kwamba maisha ya leo yana changamoto nyingi kiasi kwamba wazazi hawatangamani na watoto wao jinsi
inavyotakikana. Hali hii inaonekana kuwakera wazazi.
๐ Suala la shughuli nyingi kazini linaonekana kuhitilafiana na shughuli ya malezi. Katika sehemu hii inabainika kuwa Neema haonani na Lemi kwa sababu kila afikapo nyumbani mtoto huwa amelala.
๐ Suala la mila pia linaibuka. Wazazi wa Sara hawawezi kulala kwa mtoto wao aliyeolewa. Neema analizungumzia jambo hili kwa mshangao. Hili ni jambo la kutatiza kwa sababu mara kwa mara mamake Neema huenda mjini kwa shughuli za matibabu na huwa anahitaji mahali pa kulala.
๐ Isingekuwa kwamba Asna anaishi mjini na kwamba anaweza kumuauni mamake, basi ingempasa Neema kumkodishia chumba mamake, jambo ambalo Kiafrika ni makosa. Suala la utandawazi linajitokeza na ni dhahiri kwamba baadhi ya mila zimepitwa na wakati na zinapaswa kutupiliwa mbali kama Bela anavyoeleza:
๐ Hayo ni ya kale…na ya kale hayanuki. Wengi hawafuati tena mila hizo. Walimwengu sasa wanavaa sare moja (uk. 24). Kauli hii inaonyesha namna mabadiliko ya kijamii yamefanya baadhi ya mielekeo ya kitamaduni kupuuziliwa mbali.
Masuala makuu
Sehemu hii inadhihirisha jinsi hali za maisha ya kisasa zinavyowatatiza wanajamii. Wanalazimika kufanya kazi mchana kutwa ili kujikimu na kuzifaa familia zao. Matokeo ni kwamba hawapati nafasi ya kutangamana na familia zao ipasavyo. Ni bayana kwamba bado wanajamii wamefungwa na mila ambazo kwa hakika ni vigumu kuzitii kwa sababu ya maisha ya kisasa. Mfano mzuri ni miko inayowazuia wakwe kutolala katika makaazi ya wana wakwe zao.
Onyesho Ill
Katika onyesho hili Bunju yuko tayari kuondoka kwenda kazini asubuhi. Mazungumzo na mkewe Neema yanahusu matokeo ya mitihani ya Lemi, mtoto wao. Huku Neema akionekana kuridhishwa na matokeo hayo Bunju anamtaka Lemi kujitahidi zaidi ili apate matokeo ya kuridhisha zaidi. Mgogoro baina ya wazazi kuhusu masomo ya watoto wao unajitokeza. Hali ya Neema na Bunju kutokubaliana kuhusu bidii ya mtoto wao inaweza kuzua msukosuko.
Neema anapomwelezea Bunju kuwa mamake tayari ameshafika mjini kwa matibabu, anakataa kutoa pesa za kusaidia matibabu hayo. Bunju anadai kuwa ana majukumu mengi. Kwamba anagharamia mahitaji yote ya nyumbani, yakiwemo karo ya shule, kodi ya nyumba na amemnunulia Neema gari. Anamtaka Neema awajibike kwa sababu amemruhusu kutumia mshahara wake kwa mahitaji ya familia yake.
Bunju anasisitizia ile dhana ya kutomruhusu mama mkwe kulala nyumbani kwao. Mila na desturi hizo zinamkera Neema sana. Kwa Neema, hizo ni mila na desturi zilizopitwa na wakati.
Mtiririko wa Maonyesho Katika Bembea ya Maisha
TATHMINI
- Onyesho hili linazungumzia mambo muhimu ya kifamilia, hasa malezi na elimu. Neema anaridhishwa na matokeo ya mwanawe, ila Bunju anamtaka Lemi aongeze bidii masomoni. Hayo yakijiri, inaonekana kana kwamba ni Neema pekee anayejitahidi kushughulikia matakwa ya Lemi shuleni. Bunju analipa karo na kutekeleza majukumu mengine ila kazi yake imembana hadi hana muda wa kutangamana na familia yake ipasavyo. Mfumo wa uchumi umewagandamiza raia na kuwalazimisha kufanya kazi masaa mengi kupindukia.
- Mfumo wa elimu unawapa watoto shinikizo la kujibidiisha zaidi masomoni, jambo ambalo linaweza kusababisha msukumo wa kiakili miongoni mwa watoto. Ni bora wazazi wakiwa na msimamo mmoja kuhusu masuala yanayohusu elimu ya watoto wao.
- Mchango wa mwanamke katika ndoa unamulikwa. Bunju analipa kodi ya nyumba, karo na hata kamnunulia mkewe gari. Je, mchango wa mkewe katika
majukumu ya kifamilia ni upi? Ni muhimu mwanamke anayefanya kazi kuwekeza kiwango fulani cha pato lake katika mali ya familia ili kupata heshima na pia kama njia mojawapo ya kujifunza kuimudu familia ikiwa ataondokewa na mumewe mapema.
ONYESHO IV
Mjini, nyumbani kwa Asna. Asna anamwandalia mamake kiamshakinywa. Mama mtu anashangaa mbona bintiye anaishi katika chumba kidogo. Bintiye anajitetea kuwa chumba hicho kiko katika mtaa wa kifahari na anakifurahia. Sara analinganisha maisha ya mjini na ya kijijini na kuona kuwa yale ya mjini yanaudhi, afadhali ya kijijini.
Anasema kwamba, watu wa mjini wako mbioni kila wakati na mapato yao ni haba. Asna hakubaliani na mamake; kwake, kiwango chake cha elimu hakimruhusu kwenda kukaa kijijini. ๐ฎ Sara anamsihi Asna aolewe amletee mjukuu. Asna hakubaliani na jambo hilo. Kulingana na Asna, ndoa ina matatizo mengi kama yale anayopitia Neema, dada yake, ambaye ingawa amesoma na kupata shahada mbili, hazimsaidii kupigana na msimamo wa kitamaduni alionao Bunju, mumewe. Badala ya kupigania mabadiliko ya msimamo wa Bunju, Neema anaonekana kuukubali kwa sababu ya uhuru wa matumizi ya mshahara wake aliopewa na Bunju.
Utepetevu kazini unazungumziwa kupitia madaktari na utendakazi wao. Baadhi ya madaktari daima wako mbioni kutoka hospitali moja hadi nyingine ili kuchuma hela za ziada bila kuwazingatia wagonjwa wao kikamilifu.
MASUALA MAKUU
Kuna mambo muhimu yanayojadiliwa katika onyesho hili. Jambo la kwanza ni hadhi. Ile hali ya kutaka kuishi sehemu za kifahari hata ingawa pato ni dogo. Asna anaishi maeneo ya juu ingawa mazingira ya nyumba yake ni duni. Anajikakamua kulipa kodi ya juu ya nyumba bila kujali mazingira anamoishi.
Jambo la pili linaakisi athari za elimu ya juu dhidi ya mila na desturi za Kiafrika. Inasahaulika kwamba,elimu pekee bila uelewa haiwezi kubadilisha dhana na fikra za kitamaduni. Bunju ana elimu lakini elimu yake haijamtoa katika mila na desturi za jamii yake. Neema ana elimu lakini haimsaidii kuelewa chanzo cha mila na desturi za Bunju. Jambo la tatu ni kutosheka kwa mwanamke. Neema anaonekana kutosheka na hali ya mumewe ya kumruhusu kutumia pesa zake atakavyo. Hafikirii kuwa huenda ikawa ni mtego. Mara nyingi mwanamke anapopata uhuru wa aina hii, huweza kubugikwa na akili asiweze kufikiria kuwekeza kwa ajili ya maisha ya baadaye. Kisha mambo yanapoharibika hujikuta hana lolote la kutegemea.
Mtiririko wa Maonyesho Katika Bembea ya Maisha
Sehemu III
ONYESHO I
Nyumbani kwa Neema na Bunju. Neema yuko nyumbani anafanya usafi. Anafikiria jinsi ugonjwa wa mamake ulivyomfanya fukara. Bunju anapoingia chumbani, Neema hamsikii, anashtuka. Kwa mara nyingine, anakataa kumsaidia Neema kugharamia ugonjwa wa mamake. ๐ Anasema kwamba anafanya majukumu yote ya pale nyumbani na haoni ni kwa nini Neema hawezi kuupangia mshahara wake ili uweze
kuyakidhi mahitaji yake. Neema anahuzunishwa na msimano wa Bunju lakini pia anakumbuka maneno ya mamake kuwa Bunju ni zawadi kwake, jambo ambalo linampa heri kidogo.
Masula makuu
Onyesho hili linampa msomaji au mtazamaji nafasi ya kuelewa mahusiano katika taasisi ya ndoa. Wanandoa hao wawili wanashikana mkono kuendeleza maslahi ya jamii yao. Mume anaheshimu rai ya mkewe ya kutumia hela zake kushughulikia wazazi wake ambao ni wahitaji.
Mama ni mgonjwa na baba yake amepoteza ajira. Tofauti ya matumizi ya pesa kati ya mwanamke na mwanamume yanajitokeza. Mwanamume anajenga na mwanamke anapamba. Mambo yanapoharibika, mwanamke huachwa bila makao kwa sababu ya dhana kuwa hakuwekeza katika
ujenzi wa nyumba. Hili ni jambo linalohitaji mjadala zaidi. Bunju anajitokeza kama mwanamume anayefanya majukumu yote ya kifamilia, hali ambayo haimtayarishi mkewe kwa maisha ya baadaye iwapo mambo Kuna pia suala la matumizi ya pesa ili kutibu magonjwa. Familia nyingi yataharibika. hazina bima ya matibabu. Magonjwa yanapobisha hodi basi huziacha baadhi ya familia hizo katika hali ya umaskini. Wengi huitisha michango kama Neema anavyoitisha msaada kutoka kwa Bunju.
Katika mazungumzo yao, pia inadhihirika wazi kwamba mapato ya kazi moja hayatoshi kamwe.
Umuhimu wa kujishughulisha zaidi ili kuweza kuyamudu mahitaji unajitokeza.
ONYESHO II
Sara yuko hospitalini ambako amelazwa. Neema na Asna wamefika kumwona. Sara anataka kuruhusiwa kwenda nyumbani kwa sababu gharama ya hospitali inaendelea kupanda. Sara analinganisha huduma za matibabu za kule kijijini na za mjini. Hospitali za mjini ni kama hoteli ilhali za kijijini ni kama seli ambako mtu akilazwa hata matumaini ya kupona hudidimia.
Sara anataka atoke hospitalini arudi kijijini kwenda kumsaidia Yona ambaye alimwachia kazi zote za nyumbani. Bunju anafanya shughuli zake bila kupita hospitalini kumjulia hali Sara. Jambo hili linamkera Asna ambaye anamwona Bunju kama mchoyo na asiyewajibika kuhusu mkwe wake. Neema anamtetea Bunju.
Anasema kwamba tabia yake inatokana na jinsi alivyolelewa, kwa hivyo wasimlaumu.
MASUALA MAKUU
Mazungumzo haya yanaibua mambo matatu muhimu kuhusu hospitali aliyopรฉlekwa Sara. Mosi, malazi na chakula ni vya hali ya juu. Pili, gharama ya huduma ni ya juu mno. Tatu, hospitali hiyo ina aina nyingi za wataalamu. Hali hii inakinzana na hali ilivyo katika baadhi ya hospitali nchini ambazo ni duni na hutoa huduma mbovu zinazomfanya mgonjwa kutamauka na kukata tamaa.
Hospitali za kibinafsi hutoa mazingira mema zaidi ya kimatibabu na ni mwafaka zaidi kwa wale wanaoweza kulipia gharama zake, Mazingira ya hospitali za umma ni duni, nyingi zikiwa hazina huduma bora, hazina madaktari na hata dawa za kutosha.
Pia, mwanamume angali anapewa hadhi ya juu kuliko mwanamke. Jamii haimruhusu mwanamume kufanya kazi za jikoni kwa sababu kazi hizo huchukuliwa kuwa ni za kike. Ndiposa, ingawa Sara angali mgonjwa, bado ana ari ya kurudi nyumbani kumshughulikia Yona, mumewe.
Bunju amechorwa kama mtu asiyemjali mama mkwe. Ingawa Neema haridhishwi na hali hiyo, anashindwa kumkabili na kusingizia malezi.
Heshima anayopewa mwanamume na mwanamke katika onyesho hili, inawekwa kwenye mizani.